Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Admin.Frank Mugogo 10503

TANGAZO LA MAFUNZO KWA AJILI YA MAFUNDI NA WAENDELEZAJI WA VYANZO VYA UMEME UNAOZALISHWA KUTOKANA NA NISHATI JADIDIFU

1. Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ulianzishwa kwa Sheria Namba 8 ya Mwaka 2005 kwa ajili ya kuratibu juhudi za kuendeleza matumizi ya nishati bora vijijini. Wakala unasimamiwa na Bodi ya Nishati Vijijini (REB) ambayo pia ina jukumu la kusimamia mfuko wa Nishati vijijini (REF);

2. Jukumu kuu la Wakala ni kuhamasisha uwekezaji katika miradi ya nishati kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ambao wanahusika na huduma za jamii vijijini kama vile elimu, afya, maji n.k. sekta binafsi, asasi za kiraia na taasisi za umma. Wakala pia una jukumu la kuhamasisha matumizi ya nishati bora kwa ajili ya uzalishaji mali ili kupunguza umaskini. Aidha Wakala unashirikiana na waendelezaji wa miradi ya nishati vijijini kuibua miradi ya nishati na kujenga uwezo wa waendelezaji ili kuwa na miradi endelevu;

3. Wakala kwa kipindi cha robo ya mwisho (Aprili – Juni) ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 umepanga kutoa mafunzo ya muda wa hadi wiki mbili kwa mafundi na waendelezaji wa vyanzo vya umeme unaozalishwa kutokana na raslimali za nishati jadidifu ambayo yatafanyika katika kila mkoa Tanzania Bara. Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo mafundi na waendelezaji wa teknolojia hizi waliopo maeneo ya vijijini ili waweze kutoa huduma bora na endelevu;

4. Wakala unakaribisha maombi kutoka kwa mafundi na waendelezaji wa miradi ya nishati vijijini kutoka katika mikoa ifuatayo:
a). MARA: NISHATI ITOKANAYO NA MIONZI YA JUA - Aprili, 2017
b). GEITA: UTAYARISHAJI WA MPANGO BIASHARA - Aprili, 2017
c). TABORA: NISHATI ITOKANAYO NA MIONZI YA JUA - Mei 2017
d). SIMIYU: NISHATI ITOKANAYO NA MIONZI YA JUA - Juni 2017
e). MARA: UTAYARISHAJI WA MPANGO BIASHARA - Mei 2017
f). ARUSHA: UTAYARISHAJI WA MPANGO BIASHARA - June 2017

5. Sifa; Waombaji wawe na elimu ya kidato cha nne (wenye vyeti vya ufundi VETA daraja la 1 watapewa kipaumbele);

6. Maombi yote yatumwe yakiwa na taarifa zifuatazo:
a) Jina, anwani, namba ya simu ya atakayehudhuria mafunzo, elimu yake, kazi anayofanya na uzoefu wake; na
b) Iwapo maombi yatapitia katika taasisi/mradi wa nishati; Jina kamili la taasisi/mradi wa mwombaji, Jina la atakayehudhuria mafunzo, anwani na namba ya simu ya taasisi ikiwa ni pamoja na maelezo mafupi kuhusu uzalishaji wa chanzo husika, mahali chanzo kilipo, uwezo wake wa kuhudumia jamii au idadi ya wateja wanaotegemea kuunganishwa/kufaidika na huduma hiyo.

7. Wakala utasimamia na kugharamia mafunzo husika; na

8. Maombi yatumwe kwenye anuani ifuatayo kabla ya tarehe 17/03/2017.


Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma
S. L. P 7990
Dar es Salaam, Tanzania

Barua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007

Rate article

No rating
Rate this article:
No rating

Share

Print
«July 2024»
MonTueWedThuFriSatSun
24252627282930
1234

National Clean Cooking Strategy (2024 – 2034)

The Government of the United Republic of Tanzania, in collaboration with various stakeholders has prepared the National Clean Cooking Strategy, which provides guidance for the country’s transition to using clean cooking solutions. The strategy aims to ensure that 80 percent of Tanzanians use clean cooking solutions by the year 2034.

Please download the Strategy attached herewith.

Read more
567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930311234

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
PSSSF Building, 7th Floor
Makole Road
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top