Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Waendelezaji wa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Lupali Mkoani Njombe Waelekezwa Kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Mradi
Frank A. Mugogo 500

Waendelezaji wa Mradi wa Kuzalisha Umeme wa Lupali Mkoani Njombe Waelekezwa Kuimarisha Ulinzi na Usalama wa Mradi

Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali Mstaafu Jacob Kingu ameelekeza waendelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa kilowati 317 kwa kutumia maporomoko ya Mto Lupali kuimarisha ulinzi na usalama wa mradi ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza.

Ameelekeza hayo Juni 18, 2025 katika Kata ya Matola Wilaya ya Njombe Mkoani Njombe alipofanya ziara iliyolenga kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Mradi huo unaosimamiwa na Watawa wa Kanisa Katoliki wa Shirika la Wabenediktini, Imiliwaha Njombe kwa ufadhili wa REA.

"Mradi huu hadi kufikia hatua hii umetumia gharama kubwa, na ni mradi utakaokuwa na manufaa makubwa kwa wananchi wa maeneo haya na Taifa kwa ujumla, tuna kila sababu ya kuhakikisha unalindwa," alielekeza Mhe. Balozi Kingu.

Alielekeza kujengwa kwa uzio utakaozunguka bwawa la kuzalishia umeme sambamba na kusimika mifumo ya taa na kamera maalum za ulinzi maarufu kama CCTV Camera maeneo yote muhimu ya mradi.

Sambamba na hilo, Mhe. Balozi Kingu aliwapongeza kwa hatua waliyofikia na aliwaelekeza waendelezaji wa mradi huo kushirikiana kwa karibu na waendelezaji wa miradi mingine ili kubadilishana uzoefu katika usimamizi wa miradi.

"Hapa mmezungukwa na waendelezaji wa miradi ya namna hii wenye uzoefu, ni vyema mkajenga utaratibu wa kuwa mnabadilishana uzoefu ili kuimarisha uendeshaji wa mradi," alisisitiza Mhe. Balozi Kingu.

Akizungumza katika ziara hiyo, Mratibu wa Mradi, Sista Imakulata Mlowe alitoa shukran kwa uwezeshwaji unaofanywa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na aliahidi kusimamia maelekezo yote yaliyotolewa na Mhe. Balozi Kingu.

"Tangu kuanza kwa mradi mwaka 2011, REA imetuwezesha sehemu kubwa katika hatua zote; tunaahidi kutimiza maelekezo yote yaliyotolewa," alisema Sista Mlowe.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mhandisi Advera Mwijage alisema hadi sasa REA imewezesha zaidi ya shilingi bilioni 4.5 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi.

"REA imetoa ruzuku kwa awamu tofauti kwa kushirikiana na wabia wa maendeleo wakiwemo benki ya Dunia na Serikali ya Sweden ili kuwezesha mradi huu tangu hatua za mwanzo za utafiti wa awali, ujenzi wa njia kuu za kusafirisha na kusambaza umeme kwa watumiaji takriban 600.

Mhandisi Advera alibainisha maeneo mengine yaliyowezeshwa na REA kuwa ni pamoja na ruzuku iliyotolewa kukamilisha mradi ikihusisha ujenzi wa sehemu ya kupokelea maji, nyumba ya mtambo, uwekaji wa mabomba pamoja na shughuli nyingine za Mradi.

Alisema kukamilika kwa mradi kutazalisha kiasi cha kilowati 317 ambazo kiasi zitatumiwa na mwendelezaji na kiss kitakachobaki zitaingizwa katika Gridi ya Taifa.

Alisema kuwa REA imeendelea kufadhili mirdi ambayo itaongeza wigo wa Gridi ya Taifa ili kukuza uchumi wa Taifa kwa kuongeza kasi ya maendeleo kwa wananchi.

"REA imefadhili miradi ya uzalishaji na usambazaji nishati vijijini inayotekelezwa na taasisi mbalimbali za Serikali na Sekta Binafsi kwa kutoa ruzuku pamoja na kuwezesha mikopo ya masharti nafuu sambamba na kuwajengea uwezo waendelezaji wa miradi," alisisitiza Mha. Mwijage.

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top