Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Wananchi Wanayo Matumaini Makubwa na REA – Mhandisi Saidy
Mohamed Saif 153

Wananchi Wanayo Matumaini Makubwa na REA – Mhandisi Saidy

Awataka watumishi kufanya kazi kwa Bidii, Uadilifu na Maarifa

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi, Hassan Saidy amesema Wananchi hususan wanaoishi vijijini wana matumaini na Serikali kupitia REA katika kuwaboreshea hali ya maisha na amewataka Watumishi wa Wakala kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii, uadilifu na maarifa ili kutimiza malengo ya Serikali kuhudumia wananchi wake.

Ametoa rai hiyo Machi 12, 2026 mkoani Morogoro wakati wa kufungua Kikao cha Tatu cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa REA lenye ajenda kuu ya Kupitia na Kujadili Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2026/2027.

"Watumishi wenzangu mnafanya kazi nzuri, tuendelee kuhakikisha tunawatumikia wananchi, matumaini yao kwetu ni makubwa na leo hii tupo hapa kujadili Mapato na Matumizi katika kutekeleza na kukamilisha miradi na kwa bajeti ya REA imezingatia vipaumbele vya Serikali ikiwemo kuharakisha kupeleka umeme vitongojini, kuongeza idadi ya wateja na kutanua wigo upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia,” amesema Mhandisi Saidy.

Amesema makadirio ya Mapato na Matumizi ya Bajeti kwa Mwaka 2026/2027 yanayojadiliwa katika Baraza hilo yamelenga kuboresha mazingira ya kazi na uwezo wa Taasisi katika kutekeleza majukumu yake sambamba na maslahi ya Watumishi.

Akizungumzia mafanikio yaliyofikiwa ndani ya kipindi cha miezi 12 (kutoka kikao cha Baraza kilichopita cha Mwezi Machi, 2025 hadi kikao cha sasa Machi, 2026), Mha. Saidy amesema REA imefanikiwa kusambaza umeme kwenye vitongoji 3,532 ambayo ni sawa na wastani wa vitongoji 10 kwa siku.

"Ndani ya kipindi cha miezi 12 tumefanikiwa kusambaza mitungi 400,000, majiko banifu 300,000, kujenga mifumo ya kisasa ya kupikia kwa Taasisi 452 zinazohudumia zaidi ya Watu 100, tumeanza kutekeleza Mradi wa kupeleka Umeme - Jua kwa kaya takriban 20,000 katika visiwa 143 na ndani ya kipindi hiki miradi takriban mitatu ya kusambaza ùmeme imekamilika,” amesema Mkurugenzi Mkuu wa REA.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya Tanzania (TUGHE), Hery Mkunda ameipongeza REA kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa weledi na uzalendo.

“REA mnafanya kazi kubwa sana, mmefanikisha azma ya Serikali ya kubadilisha na kuboresha maisha ya wananchi wa maeneo ya vijijini, kwa hili kila mwananchi anaetoka kijijini ni shahidi,” amepongeza Mkunda.

Kikao cha Tatu cha Baraza la Pili la Wafanyakazi wa REA kilihudhuriwa na Mwakilishi wa Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Wilson Nyamanga, Mwakilishi wa Msajili wa HAZINA, Gerald Nzalalila pamoja na Katibu Mkuu wa TUGHE mkoa wa Dodoma, Samwel Nyangwa ambao walipata fursa ya kuzungumza na Watumishi.

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top