Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Waziri Ndejembi Aipongeza REA
Mohamed Saif 128

Waziri Ndejembi Aipongeza REA

Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuendelea kutekeleza azma ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi wake hususan wa maeneo ya vijijini  kupitia Usambazaji wa Nishati ya Umeme pamoja na Nishati Safi ya Kupikia.

Ametoa pongezi hizo Aprili 20, 2026 Jijini Dodoma alipotembelea Banda la REA katika Maonesho ya Wiki ya Nishati yanayoendelea ndani ya viwanja vya Bunge Jijini Dodoma

"Hongereni sana wataalam mnatekeleza kwa vitendo dhamira ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuwafikishia wananchi wake kote nchini Nishati," amepongeza Mhe. Ndejembi

Aidha, Mhe. Ndejembi amewaalika Waheshimiwa Wabunge kutembelea Banda la Maonesho la Nishati ili kushuhudia kazi kubwa inayotekelezwa na Wizara ya Nishati pamoja na Taasisi zake.

"Tunawakaribisha Waheshimiwa Wabunge kutembelea Maonesho haya pamoja na wageni wao kwani ni fursa nzuri ya kukutana na wataalam na Kujadili hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi katika Majimbo yao," amesema Mhe. Ndejembi.

Amesema Taasisi zote zilizo chini ya Wizara ya Nishati zinashiriki na kwamba wataalam wapo tayari na ni fursa kwa Wabunge kukutana na wataalam hao ili kujadili changamoto zilizopo na kutazama namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.

"Lengo la Maonesho haya ni kuonyesha kazi kubwa iliyofanywa na Serikali ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuna mengi ya kujifunza kwenye banda hili," amesema Mhe. Ndejembi

Halikadhalika, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy amemhakikishia Waziri Ndejembi kuwa, miradi yote inayotekelezwa kwa sasa itakamilika kwa wakati na REA imejipanga kikamilifu kutekeleza miradi hiyo. 

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ni miongoni mwa Taasisi zinazoshiriki katika Maonesho hayo yaliyoanza tarehe 20 Aprili, 2026.

 

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top