Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Zaidi ya shilingi bilioni 127.7 Zatumika Kufikisha Nishati Vijijini Mwanza
Iddy Mwema 110

Zaidi ya shilingi bilioni 127.7 Zatumika Kufikisha Nishati Vijijini Mwanza

Zaidi ya shilingi bilioni 127.7 zimetumika kupeleka huduma ya nishati safi Vijijini Mkoa wa Mwanza hali iliyochochea ukuaji wa uchumi na kuboreka kwa huduma za kijamii vijijini.

Hayo yamesemwa leo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mtanda wakati wa kikao cha kwanza kati ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Wabia wa Maendeleo katika Sekta ya Nishati (EDPG) ambapo Wakala huo uliwasilisha mpango kazi pamoja na bajeti kwa mwaka wa fedha wa 2026/2027.

 

“Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkoa wa Mwanza pekee imetoa jumla ya shilingi Bilioni 127.7 ili kutekeleza miradi ya kupeleka umeme hadi vitongojini. Mafanikio haya makubwa yamechangiwa pia na wabia wa maendeleo, tunawapongeza na kuwashukuru sana.

 

Niendelee kuwataka wananchi waendelee kulinda miundombinu ya umeme kwa kuwa serikali na wabia hawa wa maendeleo wanaweka fedha nyingi sana. Lakini pia niendelee kuwahimiza wabia wa maendeleo pamoja na REA kuendelea kuwekeza zaidi katika nishati safi ya kupikia,” amesema Mhe. Mtanda.

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali (mstaafu), Jacob Kingu amesema kuwa wabia hao wa maendeleo wamekuwa na imani kubwa na fedha wanazotoa katika utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini na ndio maana wanaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania kupitia REA katika utekelezaji wa miradi hiyo huku akiahidi kuwa Bodi yake itaendelea kuhakikisha kunakuwa na thamani ya fedha katika miradi inayotekelezwa na REA.

 

Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy amesema kuwa Wakala umewasilisha mipango na vipaumbele vyake kwa mwaka ujao wa fedha ili wabia hao waweze kuona maeneo wanayoweza kuendelea kushirikiana na Serikali kupitia REA katika kuendelea kuboresha maisha ya Wananchi.

 

“Pamoja na kazi kubwa inayofanyika katika kujenga miundombinu ya umeme, lakini lengo la msingi ni mwananchi wa kawaida aweze kuunganishiwa umeme na aweze kupata manufaa ya upatikanaji wa umeme.

 

Tumewasilisha mipango pamoja na vipaumbele katika bajeti yetu ijayo ambapo ni kuharakisha upatikanaji wa umeme kwenye vitongoji. Tumewapitisha pia wenzetu katika mpango wetu maalum wa kuwezesha na kuharakisha uunganishaji umeme majumbani,” amebainisha Mhandisi Saidy.

 

Mhandisi Saidy pia ameongeza baadhi ya mipango mingine iliyopangwa kutekelezwa na Wakala kwa mwaka ujao wa fedha ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa nishati safi ya kupikia vijijini, kuwezesha miradi ya nishati jadidifu na kuongeza ufanisi katika matumizi ya umeme na utumiaji wa umeme katika shughuli za maendeleo.

 

Mwenyekiti wa Wabia wa Maendeleo katika Sekta ya Nishati (EDPG), Robert Hovde ameipongeza Serikali ya Tanzania kupitia REA kwa kufikisha umeme vijijini.

 

“Katika kipindi cha miongo kadhaa nyuma, Tanzania imekuwa na maendeleo makubwa katika kufikisha umeme vijijini yaliyotekelezwa na REA. Miundombinu ya umeme inaonekana hali inayotia matumaini kufikiwa kwa mpango wa kuunganisha umeme wananchi wote. Tunawatakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yenu,” amesema Hovde.

 

 

 

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14
REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuwezesha waendelezaji wadogo wa miradi ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower) katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kutoa fedha, msaada wa kitaalamu na mafunzo, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa nishati nchini.

Read more
151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top