Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeibuka na ushindi wa pili katika kundi la Wakala wa Serikali katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa vijiji kulinda miundombinu ya usambazaji wa umeme katika vijiji vyao ili kuepusha hasara ambayo Serikali inapata kutokana na uharibifu wa miundombinu hiyo.
WAZIRI WA NISHATI MHE. DKT. MEDARD MATOGOLO CHANANJA KALEMANI (MB.) AMEWASILISHA BUNGENI LEO, TAREHE 08 MEI, 2020 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2020/21
Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini imekutana wa Wakandarasi wa Mradi wa REA Awamu ya III Mzunguko wa I katika Ukumbi wa Hazina, Dodoma kujadili changamoto mbalimbali zinazoweza kuchelewesha utekelezaji wa Mradi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, tarehe 06/04/2019 amezindua Mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea. Jumla ya wateja wa awali 22,700 wanatarajiwa kuunganishiwa na huduma ya umeme kupitia Mradi huu kwenye vijiji 122.