Wakala wa Nishati Vijijini unakaribisha maombi ya mkopo nafuu kuwezesha ujenzi wa vituo vidogo vya kuuzia bidhaa za mafuta (petroli na dizeli) vijijini. Mkopo huu utasaidia uwezeshaji wa ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu maeneo ya vijijini ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya mafuta kwa gharama nafuu, kwa njia salama, na isiyo na madhara kwa mazingira.
Wakala unawasisitiza waombaji walioomba katika awamu ya kwanza na kutokidhi vigezo kuomba tena baada ya kufanya marekebisho ya mapungufu yaliyobainishwa katika maombi yao. Aidha maombi mapya ya mkopo yanakaribishwa.