Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Kaya 3,255 kunufaika na majiko ya gesi ya ruzuku Wilaya ya Mlele
Frank A. Mugogo 1038

Kaya 3,255 kunufaika na majiko ya gesi ya ruzuku Wilaya ya Mlele

Wananchi Kijiji cha Usevya Wilaya ya Mlele Mkoani Katavi wamepongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kuhakikisha wanafikiwa na nishati safi ya kupikia kwa bei ya ruzuku.

Wametoa pongezi hizo kijijini hapo Agosti 12, 2025 wakati wa zoezi la usambazaji wa majiko ya gesi (LPG) ya kilo sita na vichomeo vyake kwa bei ya ruzuku ya shilingi 19,500 kwa kila jiko.

"Tunaishukuru Serikali kwa kutuletea majiko haya yanakwenda kurahisisha maisha yetu, majiko haya pia ni mkombozi wa mazingira naamini ukataji wa miti unakwenda kupungua," alisema Davis Majaliwa Mkazi wa Usevya.

Kwa upande wake Christina Sindano mkazi wa Kijiji cha Usevya alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele katika kampeni hiyo ambayo alisema inanufaisha wananchi wake hususan kina mama.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Usevya, Focus Kapongwa alisema wananchi kijijini hapo wamekuwa na mazoea ya kukata miti kwa ajili ya kuni na mkaa lakini kufika kwa mradi kutapunguza ukataji holela wa miti.

"Tunashukuru kwa hii huduma, tumepata shida sana kwenye ununuzi wa mkaa kwani sasa hivi mkaa ni bei ghali na haya majiko yatatusaidia kupunguza gharama ya maisha," alisema Kapongwa.

Akizungumza kuhusu mradi, Mtaalam wa Jinsia na Nishati wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Dkt.Joseph Sambali alisema mradi huo kwa Mkoa wa Katavi unatekelezwa kwa kushirikiana na Kampuni ya Taifa Gas Limited ambapo jumla ya majiko 3,255 ya gesi (LPG) ya kilo sita ikiwa na mafiga viwashia vyake yatasambazwa kwa bei ya ruzuku katika kila wilaya ya Mkoa wa Katavi. 

"Majiko haya yanauzwa kwa bei ya ruzuku gaharama zingine zimebebwa na Serikali lengo ni kuhakikisha nishati safi ya kupikia inapatikana kwa gharama nafuu ambayo kila mwananchi anamudu," alisema Dkt. Sambali.

Alisisitiza kuwa kila mwananchi anapaswa kuwa na kitambulisho cha Taifa (NIDA) ili kuepuka watu kujirudia kwani dhamira ni kufikiwa kwa kila mwananchi.

Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Mlele, Yahaya Mbulu alitoa wito kwa wananchi kuchangamkia fursa zinazotolewa na Serikali ikiwemo ya nishati safi ya kupikia.

"Serikali inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka kipaumbele kwenye Niishati Safi ya kupikia; inakadiriwa kuwa takribani watu 31,000 hufariki dunia kila mwaka kutokana na matumizi ya nishati isiyo salama," alibainisha Mbulu.

Alitoa wito kwa wananchi kuacha kuharibu mazingira kwa kukata miti badala yake wachangamkie fursa hiyo ya majiko ya gesi kwa bei ya ruzuku.


Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
1213141516
REA Yafadhili Mradi wa Taa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza

REA Yafadhili Mradi wa Taa Chuo Kikuu cha St. Augustine (SAUT) Mwanza

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) uko katika hatua za mwisho kukamilisha mradi mkubwa wa ufungaji wa taa 214 za barabarani katika Chuo Kikuu cha St. Augustine cha Tanzania (SAUT); Jijini Mwanza, hatua itakayoboresha mazingira ya usalama na kujifunzia kwa wanafunzi 13,600. Mradi huo unaoangazia barabara na maeneo ya chuo kwa urefu wa kilomita 6.42, unalenga kujenga mazingira rafiki na yenye ubora wa hali ya juu ili kuwawezesha wanafunzi kuendelea na masomo yao kwa urahisi wawapo chuo hapo, hususan nyakati za jioni na usiku.

Read more
1718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top