Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Lesotho Wavutiwa na REA
Frank A. Mugogo 649

Lesotho Wavutiwa na REA

Serikali ya Lesotho imevutiwa na namna ambavyo Serikali ya Tanzania kupitia Wakala wa Nishati Vijijiji (REA) imepiga hatua katika suala zima la usambazaji wa nishati safi maeneo ya vijijini.

Hayo yamebainishwa Mei 27, 2025 Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Nchini Lesotho, Tankiso Phapano akiwa ameambata na ujumbe wa wataalam katika Sekta ya Nishati nchini humo.

"Tumefuatilia kwa karibu katika suala la Nishati, Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizopiga hatua na zilizofanikiwa kwa upana wake na tupo hapa leo hii kubadilishana uzoefu na kujifunza siri hii ya mafanikio iliyowafikisha hapa," alisema Phapano.

Alipongeza jitihada binafsi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika suala la uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wake.

Akizungumzia hali ya usambazaji wa nishati maeneo ya vijijini nchini Lesotho, Meneja Kitengo cha Umeme Vijijini (REU), Leloko Mokhutsoane alisema kwa sasa nchini humo, suala la usambazaji wa umeme maeneo ya vijijini linasimamiwa na kitengo kilicho ndani ya Shirika la Umeme la Lethoso (LEC).

Alisema kutokana na kusuasua kwa ufanisi wa kitengo hicho pamoja na mahitaji ya nishati safi ya kupikia hisusan maeneo ya vijijini nchi hiyo inakwenda kuanzisha Wakala wa Nishati Vijijini.

"Hiki ni kitengo tu tena kinahusika na umeme peke yake na sio nishati kwa upana wake; kwa sasa nasi tunataka kuwa na Wakala wa Nishati Vijijini kama ilivyo hapa Tanzania ili suala la nishati safi nalo liingie na tusijifungie kwenye umeme tu," alisema Mokhutsoane.

Akizungumzia uendeshaji wa shughuli za Wakala hapa nchini kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi Hassan Saidy, Mkurugenzi wa Umeme Vijijini, Mhandisi Jones Olotu alieleza historia ya wakala hadi kufika sasa.

Mhandisi Olotu aliueleza ujumbe huo namna ambavyo REA ilianzishwa, mafanikio iliyopata hadi sasa sambamba na mipango inayoendelea kutekelezwa.

"REA Tanzania ilianzishwa rasmi mwaka 2007 na wakati huo vijiji 506 pekee vilikuwa vimefikiwa na umeme kati ya vijiji 12,318," alifafanua Mha. Olotu.

Aidha, Mha. Olotu alieleza kuwa Tanzania Bara ina jumla ya vitongoji 64,359 ambapo hadi sasa vitongoji 33,657 sawa na asilimia 52.3 tayari vimeshafikishiwa umeme.

Aliongeza kuwa, upelekaji wa umeme katika vitongoji 30,702 unaendelea ambapo vitongoji 7,736 vipo katika miradi inayoendelea na vitongoji 9,000 REA ipo katika hatua ya ununuzi wa wakandarasi ambao inatarajiwa kukamilika mwezi Juni 2025.

Aliueleza ujumbe huo kuwa hadi kufikia mwaka huu 2025 vijiji vyote 12,318 vimefikishiwa nishati ya umeme na sasa kazi inayoendelea ni kufikisha umeme katika vitongoji.

Ujumbe huo ulipata wasaa wa kujadiliana na wataalam kutoka REA masuala mbalimbali ya uendeshaji wa shughuli za Wakala.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«February 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2627
Rais Samia Apeleka Neema ya Umeme Katika Vitongoji Lindi

Rais Samia Apeleka Neema ya Umeme Katika Vitongoji Lindi

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa shilingi bilioni 25.8 wa kusambaza umeme katika vitongoji 159 utakaonufaisha kaya 5,116 Mkoani Lindi.

Read more
2829
Shangwe Mtwara - Bilioni 15.3 Kusambaza Umeme Vitongoji 175

Shangwe Mtwara - Bilioni 15.3 Kusambaza Umeme Vitongoji 175

Wananchi wa vitongoji vya Msokole na Funguni Kijiji cha Mnazi Kata ya Nalingu Mkoani Mtwara wameishukuru Serikali kwa kuwapelekea mradi wa Umeme unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ambao wamesema unakwenda kubadili maisha yao.

Read more
3031
Mkandarasi Northern Engineering Atakiwa Kuongeza Kasi Ya Ujenzi Wa Mradi Mtwara

Mkandarasi Northern Engineering Atakiwa Kuongeza Kasi Ya Ujenzi Wa Mradi Mtwara

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemtaka Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Kusambaza umeme katika Vitongoji 150 vya Majimbo 10 Mkoani Mtwara kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha Mradi kwa wakati.

Read more
1
2
Ukaguzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Mkoani Ruvuma

Ukaguzi wa Mradi wa Kusambaza Umeme Mkoani Ruvuma

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umemtaka Mkandarasi Kampuni ya CCC International Engineering Nigeria Ltd anayetekeleza Mradi wa Kusambaza umeme katika Vitongoji 135 vya Majimbo 9 ya uchaguzi Mkoani Ruvuma kuongeza kasi ya ujenzi ili kukamilisha Mradi huo kwa wakati.

Read more
345678
9101112131415
16171819202122
2324252627281
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top