Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yahamasisha Wananchi Kutumia Mkaa Mbadala
Frank A. Mugogo 1286

REA Yahamasisha Wananchi Kutumia Mkaa Mbadala

Wakala wa Nishati Vijijini unahamasisha wananchi kote nchini kutumia nishati safi ya kupikia ikiwemo Mkaa mbadala ambao umeelezwa kuwa na gharama nafuu na ni salama kwa afya ya mtumiaji na mazingira.

Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala, Mhandisi Advera Mwijage kutoka REA ametoa wito huo Mei 31, 2025 alipotembelea na kukagua uzalishaji wa mkaa mbadala unaotokana na mabaki ya makaa ya mawe katika kiwanda cha Rafiki Briquettes kinachomilikiwa na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) kilichopo Wilaya ya Kisarawe Mkoani Pwani.

"Watanzania tusiogope mabadiliko katika matumizi ya nishati safi mbalimbali za kupikia. Mkaa unaozalishwa kutokana na mabaki ya makaa ya mawe ni salama kiafya,safi na nafuu sana katika matumizi. Katika ziara hii nimetembelea hapa nimejiridhisha pasi na shaka mkaa huu ni salama kutokana na teknolojia inayotumika katika utengenezaji," alisisitiza Mhandisi Advera.

Alisema REA inatekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia na miongoni mwa majukumu iliyopewa ni kuhamasisha na kuwezesha uzalishaji, usambazaji wa bidhaa za nishati safi ya kupikia ili kila mwananchi afikiwe na amudu gharama zake.

Alisema ametembelea kiwanda hicho ili kushuhudia hali ya uendeshaji wake, kujionea uzalishaji wa mkaa mbadala ili kuwaondolea baadhi ya wananchi dhana iliyojengeka miongoni mwao ya kwamba mkaa huo si salama na pia kuona namna ambavyo serikali kupitia REA itaendelea kuwezesha uzalishaji wa mkaa huo.

"Hapa ninavyozungumza tayari tumepokea maombi kutoka STAMICO ya kuwawezesha kununua mitambo mingine ili waweze kutanua wigo wa uzalishaji, nimeridhishwa na kazi inayofanyika na sisi REA tunaahidi kuendeleza ushirikiano ili kufikia lengo na dhamira ya Serikali inayoongozwa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan," alifafanua Mha. Advera.

Alishauri STAMICO kushirikiana na vyombo vya habari na makundi mbalimbali katika jamii katika kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mkaa huo ili kuondoa dhana hiyo mbaya miongoni mwa jamii.

Akizungumzia malengo na hali ya uzalishaji, Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO, Deusdedith Magala alisema kiwanda hicho kinao uwezo wa kuzalisha kiasi cha tani 20 kwa saa na kwamba mbali na kiwanda hicho cha Kisarawe, STAMICO inamiliki viwanda vingine viwili kimojawapo kikiwa Dar es Salaam eneo la Tirdo na kingine Kiwira kulipo na malighafi hiyo ya makaa ya mawe.

"Lengo letu ni kuwa na viwanda 21 Tanzania Bara ili kurahisisha ufikishaji wa bidhaa kwa wananchi kwa gharama ambayo kila mwananchi anamudu, kwa sasa kilo moja ya mkaa kwa bei ya rejareja tunauza kwa shilingi 1,000 na kwa bei ya jumla ni shilingi 800," alisema Magala.

Alisema viwanda viwili viko mbioni kukamilika kimoja kinajengwa Mkoani Dodoma na kingine kinajengwa Mkoani Tabora kwa lengo la kupunguza ukataji ovyo wa miti unaofanywa na wakulima wa tumbaku mkoni humo wakati wa kukausha zao hilo," alisema Magala.

Naye Mhandisi Muendeshaji wa kiwanda hicho, Goodluck Mhagama alisema mkaa huo ni rahisi ikilinganishwa na mkaa wa miti kwani kilo moja inaweza kutumika kupikia kwa zaidi ya Saa 4 bila kupunguza ukali wake.

"Kilo moja ya mkaa huu unaweza kupikia maharagwe, nyama, wali ama kusonga ugali na hata kuchemsha maji bila kuongeza mkaa mwingine, wewe kazi yako ni kubadilisha tu sufuria," alsema Mhandisi Mhagama.

Alisema uandaaji wa mkaa huo umezingatia vigezo vyote muhimu na kwamba mkaa huo ni salama na hauna madhara yoyote kwa mtumiaji ama kwa mazingira na kwamba umethibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top