Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Maandalizi ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi Afrika (Mission 300) Yafikia Asilimia 95- Dkt.Biteko
Frank A. Mugogo 94

Maandalizi ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi Afrika (Mission 300) Yafikia Asilimia 95- Dkt.Biteko

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.Dkt.Doto Biteko amesema kuwa maandalizi ya Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika wenye lengo la kuharakisha upatikanaji umeme kwa Waafrika milioni 300 ifikapo 2030 (Mission 300) utakaofanyika tarehe 27 na 28 Januari jijini Dar es Salaam yamefikia asilimia 95.

Dkt.Biteko amesema hayo tarehe 15 Januari 2025 mara baada ya kukagua maandalizi ya Mkutano huo katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam akiwa ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila.

Amesema Wakuu wa Nchi 54 kutoka Bara la Afrika  wanatarajiwa kushiriki  pamoja na  viongozi wengine ambao  ni Mawaziri wa Fedha na Nishati kutoka barani Afrika, Marais wa Benki ya Dunia (WB) na Benki ya Maendeleo Afrika (AfDB), pamoja viongozi kutoka Jumuiya ya Ulaya na Jumuiya ya Umoja wa Afrika ambapo kazi zinazoendelea kwa sasa ni pamoja na kukamilisha ukarabati wa ukumbi wa JNICC.

“Kazi nyingine zinazoendelea ni pamoja na usajili na uthibitisho wa wageni ambao watakuja kwa ajili ya ushiriki na ukarabati wa maeneo mengine yatakayotumika kwenye mkutano huu, nichukue nafasi hii kuupongeza uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa hatua iliyofikiwa na kuliweka jiji kwenye mandhari ya kuvutia.” Amesema Dkt.Biteko

Ameongeza kuwa, Mkutano wa M300  umekuwa kivutio ambacho kimewashawishi  Wakuu wa Taasisi nyingi za Kimataifa kuonesha nia ya kushiriki mkutano huo mkubwa katika Sekta ya Nishati.

Ameeleza kuwa, Tanzania kuwa mwenyeji wa mkutano huo kumetokana na Diplomasia nzuri ya Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo imezidi kuimarisha uhusiano wa Tanzania kimataifa na kupelekea WB na AfDB kuichagua Tanzania kuwa mwenyeji wa Mkutano.

 Ametaja sababu nyingine ya Tanzania kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa mkutano huo muhimu ni mafanikio yaliyofikiwa katika sekta ya Nishati huku akitoa mfano wa mafanikio katika usambazaji wa nishati vijijini.

Amesema vijiji vyote nchini 12,318 vimesambaziwa umeme na Vitongoji 34,000 kati  ya 64,274  vilivyopo nchini,  tayari vimesambaziwa umeme.

Ametaja baadhi ya faida za mkutano huo kuwa ni pamoja na kuongezeka idadi ya  Watanzania watakaounganishwa na umeme ifikapo mwaka 2030 hadi kufikia milioni 13.5 kutoka milioni 5.2 ya sasa.

Ameongeza kuwa, katika mkutano huo nchi zitasaini mikakati ya kuharakisha kusambaza umeme kwa wananchi ambayo itaeleza kwa kina hatua gani zitachukuliwa chini ya mwavuli wa WB na AfDB. 

Ameongeza kuwa, faida nyingine zitakazotokana na mkutano wa M300 ni kuongezeka kwa fursa za uwekezaji, kuimarisha biashara na kuongeza heshima ya nchi katika Duru za kimataifa na Tanzania kuwa Taifa linalopigiwa mfano kwenye nyanja mbalimbali.

Dkt. Biteko ametoa wito kwa Watanzania kuupokea kwa mikono miwili mkutano huo ambao kwa kiasi kikubwa unazidi kumheshimisha Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Watanzania kwa ujumla. 

Aidha, ametoa wito kwa wananchi kuendelea na hali ya amani na utulivu kuelekea katika mkutano huo wa kihistoria kutoka nchi ipige hatua kwenye Sekta ya Nishati kwani ni Mkutano Mkubwa wa kwanza kufanyika.

 Vilevile ametoa wito kwa Waandishi wa Habari kuutangaza Mkutano huo kwa Watanzania ili waufahamu kwa kina na kufahamu fursa zilizopo.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema maandalizi ya kupokea ugeni huo yako katika hatua za mwisho.

Amesema ili kufanikisha mkutano huo, baadhi ya mitaa itafungwa ili kuwezesha  maonesho na utalii wa ndani ikiwa ni pamoja na utalii wa tiba.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«April 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
311234
CALL FOR PROPOSAL - Supply and Installation of Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions

CALL FOR PROPOSAL - Supply and Installation of Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions

The Rural Energy Agency issue the Second Call for applications from qualified suppliers to Supply and install Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions through on-call basis.

Read more
56
789
Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24

Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24

Please find the attached Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24:

Read more
10111213
14
Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania Kuboresha Maisha ya Wananchi

Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania Kuboresha Maisha ya Wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego amuopengeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi kubwa ya kufikisha umeme vijijini hali iliyobadili maisha ya wananchi vijijini.

Read more
151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top