Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi
Frank A. Mugogo 201

Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini Mkoani Lindi.

Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi REA, Mhandisi Emanuel Yesaya amebainisha hayo Januari 3, 2025 Mkoani Lindi wakati wa kumtambulisha mtoa huduma huyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.

"Ili kufikia azma ya Serikali kupitia Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ya kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati kupikia; REA tumekuja na programu hii ya kusambaza majiko ya gesi ya kilo sita kwa bei ya ruzuku," alisema Mhandisi Yesaya.

Alisema kuwa lengo la mradi huo ni kukuza, kuchochea, kuwezesha na kuboresha upatikanaji wa huduma za Nishati Safi ya kupikia ili kupunguza ukataji miti. 

"Mradi huu unakwenda kusaidia kuondokana na athari za kiafya, pia utasaidia kuepuka vitendo vya kikatili, kulinda vyanzo vya maji na kutunza Mazingira na pia kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabia ya nchi," alifafanua Mhandisi Yesaya.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Zuwena Jiri amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mradi huo wa majiko ya ruzuku ambao alisema utaongeza matumizi ya nishati safi kupikia hususan kwa wananchi wa maeneo ya vijijini. 

"Tumefurahi kupata mradi huu;  tunamshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na tutaendelea kuhamasisha wananchi kuachana na matumizi ya nishati zisizo kuwa safi na salama ili kulinda afya na mazingira," alisema.

Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kujaza mitungi pale inapoishiwa gesi ili kuendelea kutumia.

Alimuelekeza Mtoa huduma (Taifa Gas) kuhakikisha anakuwa na mawakala kwenye kila kata na vijiji ili kumrahishia mwananchi kubadilisha mtungi pale gesi inapomalizika.

"Ili kuwa na uendelevu wa matumizi ya gesi kupikia, natoa wito kwa Taifa Gas kuwa na mawakala ili kumrahishia mwananchi; tusikubali kumpoteza mtu kurudi kwenye kuni na mkaa kwa sababu ya kukosa mahala pa kubadili mtungi," alielekeza. 

Kwa upande wake, Meneja   mauzo wa Taifa Gas Kanda ya Kusini, Hawa Omari alithibitisha kuwa wanejipanga vyema kufika kwenye maeneo yote Mkoani hapo sambamba na kutoa elimu kwa wananchi watakaonunua majiko hayo kabla ya kutumia.


Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«February 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
27
Mkutano wa Nishati Afrika (M300) Kuchochea Maendeleo ya Afrika

Mkutano wa Nishati Afrika (M300) Kuchochea Maendeleo ya Afrika

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika - Misheni 300 ni kichocheo cha maendeleo ya nchi za Afrika na kichocheo cha utekelezaji wa Sera yake ya Taifa ya Nishati inayolenga kuendeleza nishati endelevu, uhifadhi na ufanisi.

Read more
2829303112
3456789
1011121314
REA Yaanza Kusambaza Mitungi ya Gesi 13,020 Mkoani Songwe

REA Yaanza Kusambaza Mitungi ya Gesi 13,020 Mkoani Songwe

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na kampuni ya Oryx Gas Tanzania, tarehe 12 Februari, 2025 imeanza rasmi kusambaza mitungi ya gesi ya kilo 6 kwa wakazi wa mkoa wa Songwe na kwa kuanzia Wananchi wa wilaya ya Mbozi wameanza kununua mitungi hiyo kwa nusu bei.

Read more
1516
17181920212223
242526272812
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top