Wakala wa Nishati Vijijini (REA) katika kipindi cha Mwaka wa Fedha 2014/2015
umepanga kutoa mafunzo ya hadi wiki mbili kwa wajasiriamali wanaoendeleza vyanzo
vya umeme unaofuliwa kutokana na nishati jadidifu. Lengo la mafunzo haya ni
kuwajengea uwezo mafundi na waendelezaji wa teknolojia za nishati bora waliopo
maeneo ya vijijini ili waweze kutoa huduma bora.
Wakala unakaribisha maombi kutoka kwa mafundi na waendelezaji wa miradi ya
nishati vijijini katika teknolojia zifuatazo:
1. Nishati itokanayo na maporomoko madogo ya
maji
2. Nishati itokanayo na tungamotaka (biogas &
biomas)
3. Nishati itokanayo na upepo
4. Utayarishaji wa mpango biashara
5. Nishati itokanayo na mionzi ya jua
Sifa za Mwombaji
Waombaji wawe na elimu ya Kidato cha Nne (wenye vyeti vya ufundi VETA Daraja
la 1 watapewa kipaumbele)
Maombi yote yatumwe yakiwa na taarifa zifuatazo:
1. Jina, anwani, namba ya simu ya
atakayehudhuria mafunzo, kazi anayofanya, uzoefu wake na vivuli v ya vyeti vya
elimu aliyonayo.
2. Iwapo maombi yatapitia katika taasisi/mradi
wa nishati; Jina kamili la taasisi/mradi wa mwombaji, Jina la atakayehudhuria
mafunzo, nakala ya vyeti vya elimu aliyonayo, anwani na namba ya simu ya taasisi
ikiwa ni pamoja na maelezo mafupi kuhusu uzalishaji wa chanzo husika, mahali
chanzo kilipo, uwezo wake wa kuhudumia jamii au idadi ya wateja
wanaotegemea kuunganishwa/kufaidika na huduma hiyo.
Wakala utasimamia na kugharamia mafunzo husika. Mwombaji atatakiwa kugharamia
usafiri wa kwenda na kurudi katika mafunzo.
Maombi yatumwe kwenye anuani ifuatayo kabla ya tarehe 15/08/2014.
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma
S.L.P. 7990
Dar es Salaam, Tanzania
Parua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007