Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Mhe. Rais Samia Apongezwa Kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Vitendo
Frank A. Mugogo 603

Mhe. Rais Samia Apongezwa Kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Vitendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa vitendo.
 
Pongezi hizo zimetolewa leo Julai 1, 2025 na Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Lucas Malunde wakati akimwakilishi Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Mhe. Balozi Meja Jenerali (mstaafu), Jacob Kingu katika hafla ya kugawa mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na jiko la gesi la sahani mbili kwa Watumishi wa Magereza Mkoa wa Simiyu.
 
"Mei 8, 2024, Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan alizindua Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia. Toka kuzinduliwa kwa mkakati huo, Serikali imefanya juhudi mbalimbali kuhakikisha Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ili kuokoa mazingira pamoja na vifo vilivyokuwa vinatokana na matumizi ya nishati isiyokuwa safi na salama ya kupikia.
 
Mhe. Rais ameweza kutoa fedha zilizowezesha magereza zote nchini kuachana na matumizi ya kuni na kuanza kutumia nishati safi ya kupikia. Na leo tuko hapa kugawa mitungi ya gesi pamoja na majiko yake kwa Watumishi wa Magereza. Zote hizi zikiwa ni juhudi za Mhe. Rais kuhakikisha Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia unatekelezwa kwa vitendo," amesema Mjumbe huyo wa Bodi.
 
Awali akitoa taarifa kuhusu mradi huo, Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Wawekezaji Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Emmanuel Yesaya amesema kuwa jumla ya mitungi ya gesi ya Kilogramu 15 na majiko ya gesi ya sahani mbili 330 itagaiwa kwa Watumishi wa Magereza Mkoa wa Simiyu.
 
Kwa upande wake Mkuu wa Magereza Mkoa wa Simiyu, SACP Lugano Msomba ameishukuru Serikali kupitia REA kwa kuwawezesha Watumishi wa Magereza kupata nishati safi ya kupikia na kuahidi kuwa watakuwa mabalozi kwa wengine katika kampeni hiyo.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma
 

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top