Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yasambaza Mitungi na Majiko ya Gesi kwa Watumishi wa Gereza la Ukonga Dar es Salaam
Frank A. Mugogo 328

REA Yasambaza Mitungi na Majiko ya Gesi kwa Watumishi wa Gereza la Ukonga Dar es Salaam

Serikali imesambaza kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza (Gereza la Ukonga) mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na majiko yake 464 ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kama njia ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia nchini ambapo msisitizo ni angalau asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia Nishati Safi ifikapo Mwaka 2034.

Hafla ya ugawaji wa mitungi na majiko yake iliongozwa na Mhe. Balozi, Radhia Msuya, Mkurugenzi wa Bodi ya Nishati Vjijini (REB) katika gereza la ukonga, Jijini, Dar es Salaam, leo Juni 30, 2025 ambapo kwa upande wa Magereza uliwakilishwa na Msaidizi wa Mkuu wa Gereza hilo, Kamishna Msaidizi, (ACP); Athuman Recha.

Balozi, Radhia amesema kuwa, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Watumishi hao watasambaziwa mitungi ya gesi na majiko yapatayo 464 na kuongeza kuwa huo ni sehemu ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais wa Awamu ya Sita; Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kama nyenzo ya kulinda afya za Watanzania, kulinda na kutunza mazingira 

Amesema kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia makubaliano na Jeshi la Magereza ili kuwawezesha, kuhama kutoka katika matumizi ya nishati isiyo salama kwenda katika matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia katika magereza yote nchini. 

“Serikali kupitia REA, ilishaanza uwezeshaji kwa Jeshi la Magereza na wameshaanza kutumia Nishati Safi na kwa msisitizo huo, tuliona ni vyema, kuwawezesha Watumishi na Maafisa ili nao waachane na nishati chafu ili kulinda afya zao pamoja na kulinda mazingira yetu”. Amesema, Mhe. Balozi, Radhia.

Naye, Mkurugenzi wa Fedha na Uwezeshaji, CPA, Daniel Mungure ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), amewataka watumishi wa jeshi la magereza  kuibeba Ajenda ya Mhe. Rais Samia ya kuwa Mabalozi wa Nishati Safi ya kupikia kwa kuendelea kutumia gesi na siyo kuni na mkaa.

Akishukuru kwa uwezeshaji huo kwa Watumishi na Maafisa wa Jeshi la Magereza, Mrakibu Mwandamizi, (SSP); Moses Mumbi amesema, wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwajali na kuongeza kuwa teknolojia hizo za Nishati Safi ya Kupikia si tu zinalinda afya zao lakini zinaongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao wakati wa kuwahudumia Mahabusu na Wafungwa.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«November 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
272829303112
3456789
10111213141516
17181920212223
24252627282930
1234567

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top