Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yasambaza Mitungi, Majiko ya Gesi kwa Watumishi 461 wa Magereza Mkoa wa Mara
Frank A. Mugogo 414

REA Yasambaza Mitungi, Majiko ya Gesi kwa Watumishi 461 wa Magereza Mkoa wa Mara

Katika kuendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imegawa jumla ya mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na majiko ya sahani mbili 461 kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mara.
 
Akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji wa mitungi hiyo iliyoanza kugaiwa katika Gereza la Wilaya Musoma leo Julai 02, 2025, Mjumbe wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Lucas Malunde amesema kuwa mradi huo umelenga kuwafikia watumishi wa magereza 15,126 wote nchini.
 
Amesema kuwa, Wakala wa Nishati Vijijini uliingia makubaliano na Jeshi la Magereza Septemba 13, 2024 uliolenga kuwezesha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa Magereza yote nchini.
 
Mkataba huo wenye gharama ya Shilingi Bilioni 35.23 umelenga kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya gesi asilia, ujenzi wa miundombinu ya biogas, ujenzi wa miundombinu LPG, usambazaji wa mitungi ya gesi pamoja na majiko ya sahani mbili kwa watumishi wa magereza, usambazaji wa mkaa mbadala, ununuzi wa mashine za kutengenezea mkaa mbadala na kuwajengea uwezo watumishi wa magereza kuhusu matumizi ya nishati safi ya kupikia.
 
"Serikali kupitia REA imeweza kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia na sasa Magereza yote Tanzania Bara yanatumia nishati safi ya kupikia. Hii ni hatua kubwa sana katika kuendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.
 

Na leo tunaendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kugawa bila gharama yoyote mitungi hii ya Kilogramu 15 na majiko ya sahani mbili kwa watumishi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mara. Mkawe mabalozi wazuri wa nishati safi ya kupikia," amesema Mjumbe huyo wa Bodi.
 
Awali, Mkuu wa Magereza Mkoa wa Mara, ACP. Hospitius Mendi amesema kuwa tangu kuanza kutumia nishati safi ya kupikia, Magereza wameokoa muda waliokuwa wanatumia kutafuta kuni pamoja na gharama za kusafirisha kuni.
 
Kwa upande wake Kaimu Meneja Usaidizi wa Kiufundi kwa Wawekezaji Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Emmanuel Yesaya ametoa rai kwa watumishi wa jeshi la magereza wote nchini kutunza miundombinu ya nishati safi ya kupikia iliyofungwa katika magereza pamoja na kuwa mabalozi wa nishati safi ya kupikia.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«December 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
242526
Rais Samia Atoa Ruzuku ya Kufanya  Wiring Miradi ya Umeme Vijijini

Rais Samia Atoa Ruzuku ya Kufanya Wiring Miradi ya Umeme Vijijini

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaanza kutekeleza mradi wa kutandaza nyaya za umeme (wiring) kwa wananchi kupitia miradi ya kusambaza umeme inayotekelezwa na wakala kote nchini.

Read more
27282930
123
Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya Nishati Safi

Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya Nishati Safi

Karibu katika Hafla ya Kusaini Mikataba ya Kufunga Miundombinu ya Nishati Safi katika Shule za Sekondari 52 pamoja na Chuo cha VETA.

Read more
4567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930311234

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top