Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Mkurugenzi Mkuu REA Ahamasisha Wananchi Kutumia Nishati Safi ya Kupikia
Aodax K. Nshala 239

Mkurugenzi Mkuu REA Ahamasisha Wananchi Kutumia Nishati Safi ya Kupikia

Serikali Imetoa Ruzuku Katika Mitungi ya Gesi (LPG) Na Majiko Banifu

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amewaasa wananchi kutumia Nishati Safi ya Kupikia ili kuokoa gharama na muda, kulinda mazingira na afya zao hasa ikizingatiwa kuwa teknolojia sasa imeboreshwa na gharama yake ni nafuu ikilinganishwa na nishati zingine. 

Mhandisi Saidy ametoa rai hiyo Agosti 8, 2024 mbele ya wananchi waliotembelea Banda la REA katika Maonesho ya Siku Kuu ya Wakulima (Nane Nane), Nzuguni Jijini Dodoma. 

"Tunaendelea kuhamasisha wananchi kutumia Nishati Safi ya Kupikia kwani ni salama, rafiki na gharama yake ni nafuu kwani teknolojia sasa imeboreshwa," amesema Mhandisi Saidy. 

 Mhandisi Saidy amesema ipo dhana ambayo imejengeka katika jamii kuwa matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ni ghali na si salama na pia chakula kinachopikwa kutokana nayo hakina ladha suala ambalo alisisitiza halina kweli. 

"Ninawathibitishia Nishati Safi ya Kupikia ni salama kuliko nishati zingine tulizozizoea, niwatoe wasiwasi katika hili na tunaendelea kutoa elimu kuhusu usalama na umuhimu wa nishati hii bora," amesema Mhandisi Saidy.

Akizungumzia upatikanaji wa Nishati Safi ya Kupikia kwa wote, amesema Serikali imetoa ruzuku katika usambazaji wa Mitungi ya Gesi (LPG) na Majiko Banifu ili kuvutia wawekezaji wengi na pia kumuwezesha kila mwananchi aweze kumudu gharama zake. 

"Serikali imekuja na mfumo wa kumrahisishia kila mwananchi hususan yule mwenye kipato cha chini kumudu gharama ya Nishati Safi ya Kupikia kokote aliko ili aachane na matumizi ya nishati nyingine," amefafanua Mhandisi Saidy. 

Amesema Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameipatia REA jukumu la kuhakikisha inasimamia vyema utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 ili kufikia 2034 asilimia 80 ya wananchi wawe wanatumia Nishati Safi ya Kupikia. 

"Tunamshukuru Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuamini na kutupatia jukumu hilo kubwa na tayari kwa kushirikiana na wadau tumeanza utekelezaji wake na tunakwenda vizuri," amefafanua Mhandisi Saidy. 

Amesema hatua inayoendelea sasa ni kuibua na kuwawezesha wazalishaji wengi wa vifaa vya Nishati Safi ya Kupikia ili kuongeza umahiri sambamba na kuwawezesha kutengeneza bidhaa nyingi kwa gharama nafuu na kwa ubora wa kimataifa," amesema. 

Amesema kwa kufanya hivyo kutakuwa na ongezeko la matumizi ya nishati safi ya kupikia, ongezeko la ajira na hivyo kukuwa kwa uchumi.
 

Imetolewa na:
Mohamed M. Seif
msaif@rea.go.tz
Afisa Habari
REA

Share

Print
«January 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
678
Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini Mkoani Lindi.

Read more
9101112
13141516171819
20212223242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top