Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Rais Samia Aipongeza REA
Aodax K. Nshala 1327

Rais Samia Aipongeza REA

Atembelea Kitua Kituo cha Kupokea na Kupoza Umeme cha Ifakara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameupongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi nzuri wanazofanya.

Mhe. Rais ametoa pongezi hizo leo Agosti 4 wilayani Kilombero, Mkoa wa Morogoro alipotembelea Kituo cha Kupokea na Kupoza umeme cha Ifakara kilichojengwa na Serikali ya Tanzania kupitia REA kwa kushirikiana na Umoja wa Ulaya kilichotatua changamoto ya muda mrefu ya umeme wa uhakika katika Wilaya ya Malinyi, Ulanga na Ifakara.

Awali akitoa maelezo kuhusu mradi huo, Naibu Waziri Nishati, Mhe. Judith Kapinga amesemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia kwa kuridhia kupitia Wizara ya Nishati kujenga vituo 75 vya kupokea, kupoza na kusambaza umeme ikiwa ni jitihada zake za kuhakikisha wananchi katika maeneo yote wanapata umeme wa uhakika.

"Kabla ya mwaka 2021 nchi ilikuwa ina vituo 61 tu vya kupokea na kupoza umeme, tunakushukuru sana Mhe. Rais kwa kuridhia ujenzi wa vituo vingine vipya 75." Amesema Mhe. Kapinga

Mhe. Naibu Waziri Kapinga amesema kuwa, tayari vituo nane vimejengwa na kuanza kazi huku vituo sita vikifikia asilimia 97.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema kituo cha Ifakara kimejengwa kutokana na uhitaji mkubwa wa umeme wilayani Ifakara, Malinyi na Ulanga na hii pia inatokana na shughuli kubwa za kilimo na uchimbaji madini.

Mhandisi Hassan ameongeza kuwa, kabla ya ujenzi kituo cha Ifakara umeme kwa mwezi ulikuwa ukikatika mara 18 ambapo hivi sasa ikitokea umeme umekatika basi ni mara moja.

Ameongeza kuwa gharama ya ujenzi wa kituo hicho ilikuwa ni shilingi bilioni 24.5 ambapo serikali imechangia gharama hizo pamoja na wadau wa maendeleo ambao ni Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) na kukamilika kwa kituo hicho haujasaidia tuu kuongeza thamani ya mazao bali pia umesaidia kuboresha huduma za kijamii kama afya kwa upatikanaji wa umeme wa uhakika katika hospitali na zahanati.
 

Imetolewa na:
Iddy M. Mwema
imwema@rea.go.tz
Afisa Habari
REA

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14
REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuwezesha waendelezaji wadogo wa miradi ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower) katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kutoa fedha, msaada wa kitaalamu na mafunzo, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa nishati nchini.

Read more
151617181920
212223
Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo Mwaka 2030

Miradi Ya Kusambaza Umeme Vitongojini Kukamilika Ifikapo Mwaka 2030

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy, amesema Serikali imedhamiria kukamilisha miradi ya kusambaza umeme katika vitongoji vyote ifikapo mwaka 2030, hatua ambayo itachochea shughuli za kijamii na kiuchumi kwa wananchi.

Read more
2425
REA Yatunukiwa Cheti cha Mlipakodi Bora kwa Taasisi za Umma

REA Yatunukiwa Cheti cha Mlipakodi Bora kwa Taasisi za Umma

Wakala wa Nishati Vijijini (REA), umetunukiwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Cheti cha Mlipakodi Bora kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 kwa Taasisi za Umma, ikiwa ni kutambua kiwango bora cha Wakala katika kuzingatia taratibu za ulipaji kodi.
 

Read more
2627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top