Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA itaendelea kufanya tafiti za ufanisi wa bidhaa za nishati safi za kupikia
Frank A. Mugogo 585

REA itaendelea kufanya tafiti za ufanisi wa bidhaa za nishati safi za kupikia

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema Wakala utaendelea kufanya tafiti za bidhaa za Nishati Safi za Kupikia ili kubaini ufanisi wa teknolojia zinazosambazwa kwa wananchi.

Mhandisi Saidy amesema hayo Agosti 23, 2024 alipotembelea Banda la Wakala katika Tamasha la Kizimkazi eneo la Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

"Tutaendelea kufanya utafiti wa bidhaa mbalimbali za Nishati Safi za Kupikia ili kutimiza dhamira ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Nishati Safi ya Kupikia kwa wote inapatikana kwa gharama nafuu na yenye ufanisi," amesema.

Amesema dhamira ni kuwa na teknolojia sahihi, rafiki na yenye gharama nafuu ili kumuwezesha na kumrahisishia kila Mwananchi kuwa na bidhaa bora.

"Tutahakikisha lengo la Serikali kupitia Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia 2024-2034 la kufikisha asilimia 80 ya wananchi wanaotumia Nishati Safi ya Kupikia ifikapo 2034 linafikiwa," amesema.

Mhandisi Saidy vilevile alitembelea mabanda ya Wadau wanaojihusisha na uandaaji, uuzaji na usambazaji wa Nishati Safi ya Kupikia na kujadiliana masuala mbalimbali hususan namna bora ya kuendelea kuboresha bidhaa zao ili kuleta tija inayokusudiwa.

Awali kabla ya kutembelea  Maonesho ya Kizimkazi, Mhandisi Saidy alishiriki Kongamano la Nishati Safi ya Kupikia lililoandaliwa na Taasisi ya Mwanamke Initiatives Foundation (MIF) na Benki ya Uwekezaji ya Tanzania (TIB) kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Taasisi zake ikiwemo REA ambapo Wakala ulipata fursa ya kuelezea suala la Upatikanaji wa Fedha katika kuendeleza Nishati Safi ya Kupikia.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2829301234
56
REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

REA Yawataka Waendelezaji Miradi Ya Kuzalisha Umeme Kwa Maji Kuchukua Tahadhari Ya El Nino

Wakala wa Nishati Vijijini REA imejipanga  kuendelea kuimarisha na kuwezesha Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Kuzalisha Umeme kwa Maporomoko ya Maji, ikiwemo kuhakikisha miradi hiyo inalindwa dhidi ya athari zinazoweza kusababishwa na mvua kubwa za El Nino zinazotarajiwa kunyesha katika kipindi hiki.

Kauli hiyo imetolewa leo Oktona 6, 2026 na Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala wa REA, Mhandisi Advera Mwijage, wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya Mradi wa Umeme wa Ijangala wenye uwezo wa kuzalisha Kilowati 360, uliopo katika Kijiji cha Masisiwe, Wilaya ya Makete mkoani Njombe.

Read more
7891011
12131415161718
19202122232425
2627282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top