Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Shule za Sekondari 52; Chuo cha VETA Kufungiwa Miundombinu ya Nishati Safi
Issa Sabuni 206

Shule za Sekondari 52; Chuo cha VETA Kufungiwa Miundombinu ya Nishati Safi

Shilingi bilioni 5.8 yawezesha utekelezaji wa mradi huo

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imesaini mikataba ya kufunga miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwa shule za Sekondari 52 na Chuo cha VETA kimoja hapa nchini.

Hafla hiyo ya utiaji saini imeongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Hassan Saidy leo, Disemba 4, 2025 Jijini Dar es Salaam pamoja na Wawakilishi wa kampuni ya TAIFA Gas Ltd na Hanny G Ltd ikiwa ni sehemu ya awamu ya kwanza ya utekelezaji wa mkataba wa kuziwezesha Taasisi zinazohudumia watu zaidi ya 100 kufungiwa miundombinu ya nishati safi ya kupikia.

"Hafla ya leo ni mwendelezo wa utekelezaji wa Mkakati wa Nishati Safi ya kupikia, uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe, Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 8 Mei 2024 lakini pia na katazo la Serikali lililotolewa mwaka 2024 kuhusu matumizi ya kuni na mkaa kwa Taasisi zote zinazohudumia watu zaidi ya 100, "Amesema Mha. Saidy.

Mha. Saidy amesema, mradi huo utahusisha upelekaji wa mifumo ya nishati safi ya kupikia kwenye shule 52 za Sekondari na Chuo kimoja cha VETA ili kuendelea kuhamasisha matumizi ya nishati safi hapa nchini.

Ameongeza kuwa, mradi huo utanufaisha Waalimu 2,192, Wanafunzi 54,405 na utatekelezwa katika mikoa 18 hapa nchini. Amesema mradi huo pia ni mwendelezo wa jitihada za Serikali kupitia REA ambazo zinalenga katika kuziwezesha Taasisi mbalimbali kutumia nishati safi ya kupikia.

Naye, Mkurugenzi wa Teknolojia za Nishati Jadidifu na Mbadala kutoka REA, Mha. Advera Mwijage amesema gharama ya mradi huo ni shilingi bilioni 5.8 na wanufaika ni shule 52 za Sekondari na Chuo kimoja cha VETA.

"Mifumo itakayofungwa ni LPG ya kuanzia tani moja hadi mbili,  masufuria ya kupikia yanayotumia LPG yenye mita za ujazo 50 hadi 300 masufuria ya kupikia yenye mita za ujazo 50 hadi 300 yanayotumia mkaa mbadala, pamoja na ununuzi wa mkaa mbadala wa kuanzia kwa Taasisi zote zinazonufaika," Amesema Mha. Mwijage.

Mha. Mwijage ameeleza kuwa, Wakala ulishafunga mifumo katika shule mbili zilizopo Simiyu pamoja na Ruvuma. Ameongeza kuwa ufungaji wa mifumo ya nishati safi ya kupikia katika shule ya sekondari Ruhinda iliyopo katika mkoa wa Kagera unaendelea.

Kwa upande wake, Meneja wa Mauzo wa Taifa Gas, Mosses Massawe amemshukuru Rais Samia kwa kuona umuhimu wa kuziwezesha Taasisi mbalimbalu ili ziachane na nishati isiyo safi na salama na kuhamia katika matumizi ya nishati safi.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Hanny G Investment, Hanny Mbaria ameishukuru Serikali kupitia REA na kubainisha kuwa watatekeleza mkataba huo kikamilifu ili kuhakikisha Watanzania na Taasisi zinatumia nishati safi na salama.

MWISHO!!!

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top