Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA DODOMA
Admin.Frank Mugogo 10260

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA DODOMA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Dodoma. Mgeni rasmi Katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 16/03/2017 katika kijiji cha Kigwe Wilaya ya Bahi alikuwa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani.

Mradi huu unajumuisha vipengele-mradi vitatu vya Grid Extension, Densification ambayo inalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya vijiji na vitongoji havikuunganishiwa umeme. Kipengele-mradi cha tatu kinahusisha usambazaji wa nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi.

Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Dodoma utahusisha vipengele vyote vitatu. Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti. Sehemu ya awali itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 182 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 75. Utekelezaji wa sehemu hii ya kwanza umeanza Mwezi Februari 2017 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 2019.

Aidha, sehemu ya pili ya mradi huu wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu itaanza kutekelezwa baada ya sehemu ya kwanza kukamilika mwaka 2019 ambapo vijiji 166 vitapatiwa umeme na hivyo kufikisha umeme katika vijiji vyote vya mkoa wa Dodoma ifikapo Mwaka 2021.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma
S. L. P 7990
Dar es Salaam, Tanzania

Barua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007

Share

Print
«November 2024»
MonTueWedThuFriSatSun
28293031123
456
Zaidi ya Bilioni 11 Kusambaza Umeme Vitongojini Shinyanga

Zaidi ya Bilioni 11 Kusambaza Umeme Vitongojini Shinyanga

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa Shilingi Bilioni 11.18 wa kusambaza umeme katika vitongoji 90 utakaonufaisha Kaya 2,970 Mkoani Shinyanga.

Read more
78
REA Kufunga Mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia Shule ya Ruhinda

REA Kufunga Mifumo ya Nishati Safi ya Kupikia Shule ya Ruhinda


Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeahidi kujenga mifumo ya nishati safi ya kupikia pamoja na jiko katika shule ya Sekondari ya mchanganyiko ya Ruhinda iliyopo Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera.

Read more
910
111213

Report of the Controller and Auditor General on Financial and Compliance Audit for the Financial Year Ended 30 June 2023 for the Rural Energy Agency (REA)

Report of the Controller and Auditor General on Financial and Compliance Audit for the Financial Year Ended 30 June 2023 for the Rural Energy Agency (REA).

Read more
14
Call for Proposals to Supply Clean Cook Stoves for Promotions on Call Basis

Call for Proposals to Supply Clean Cook Stoves for Promotions on Call Basis

The Rural Energy Agency invites applications from qualified suppliers to submit proposals detailing the types of clean cooking solutions intending to supply clean cooking solutions across the country at subsidized rates. The proposal should also outline the actual costs and distribution expenses for providing these services in rural areas.

Read more
151617
18192021222324
2526272829301
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top