Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ahamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia
Frank A. Mugogo 546

Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Ahamasisha Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru wa Kitaifa, Ismail Ali Ussi amewahamasisha wananchi kuunga mkono kampeni ya nishati safi ya kupikia ili kulinda afya pamoja kuokoa mazingira.
 
Ussi ametoa wito huo jana Septemba 6, 2025 wakati wa ugawaji wa mitungi ya gesi ya kilogramu 6 zaidi ya 500 kwa wananchi wa Wilaya ya Chato, Mkoani Geita inayotolewa na Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) ikiwa ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia ambao umelenga kufikia mwaka 2034 zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati ya kupikia.
 
"Kila mmoja akawe balozi wa kampeni hii ya nishati safi ya kupikia ili tuweze kulinda afya za wananchi wetu pamoja na kuokoa mazingira yetu ambayo yameharibiwa kwa ukataji wa miti kama chanzo cha nishati ya kupikia," amesema Ussi.
 
Kwa upande wao wananchi wa Wilaya hiyo wameipongeza na kuishukuru Serikali kupitia REA kwa kuwapatia majiko ya gesi huku viongozi wa Kijiji wakiahidi kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa wananchi wao.
 
"Mimi kama Kiongozi nitaendelea kuhamasisha wananchi kuachana na matumizi ya kuni na mkaa na badala yake watumie nishati safi ya kupikia kama gesi.
 
Lakini pia nitaunda kamati ya kupita katika kila Kitongoji kuhamasisha wananchi ambao wanatumia kuni waanze kutumia nishati safi ya kupikia," amesema Juma Nzihilabike, Mwenyekiti wa Kijiji cha Musasa.
 
Kwa upande wake Mhandisi Miradi kutoka REA, Francis Manyama amesema kuwa REA inaendelea kutekeleza maono ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwamo mradi wa kugawa majiko ya gesi pamoja na majiko banifu kwa bei ya ruzuku.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«October 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
293012345
6789101112
13141516171819
20212223242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top