Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy amewapongeza Watumishi wa Wakala huo kwa kufanya kazi kwa bidii na kujituma hali iliyopelekea kukamilika kwa miradi inayotekelezwa na REA kwa wakati na katika ubora ulikusudiwa.
Mhandisi Hassan ametoa pongezi hizo leo tarehe 27 Machi, 2025 wakati akizungumza na Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi katika Mkutano wa Pili (Kikao cha Sita) cha Baraza hilo, mkoa Morogoro katika ukumbi wa Magadu.
Mha. Saidy amesema miaka minne iliyopita; Baraza la Wafanyakazi lilikuwa na idadi ndogo ya Wajumbe na ambao wengi wao walikuwa wakitoka kwenye Menejimenti, tofauti na sasa ambapo Wajumbe wengi wanatoka kwenye kundi la Watumishi wote.
“Wageni na Wajumbe wa Baraza hili ni Baraza letu la Pili, Mwezi Desemba, 2021 ndiyo tulianza Baraza letu la kwanza, napenda kuwapongeza kwa ufanisi na kujituma kwenu kwa kuwa ninyi (Watumishi) ndiyo chanzo cha mafanikio ya Taasisi yetu.”Amesema, Mhandisi, Saidy.
Mhandisi Saidy ametoa wito kwa Watumishi (Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi) kuwa huru kutoa michango ya mawazo yao kwa yale mambo ambayo yataongeza tija kwenye Taasisi (Wakala) na kwa Watumishi.
Naye Mkurugenzi wa Utawala na Rasilima Watu kutoka Wizara ya Nishati, Bi. Zaina Mlawa amesem Wizara ya Nishati (Makao Makuu) itaendelea kuzisimamia Taasisi zake zote zilizochini yake (Ikiwemo REA) ili kuendelea kuongeza tija na ufanisi kwa utoaji wa huduma kwa umma.
Kwa upande wake Mjumbe wa Baraza Kuu TUGHE Taifa, Dkt. Elias Mtungilwa ametoa pongezi nyingi kwa Baraza la Wafanyakazi la REA kwa kuwa na uwinao mzuri wa Wajumbe kutoka makundi yote Watumishi pamoja na kuzingatia masuala ya jinsia.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma