Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Yahitimisha Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Umeme Mkoani Njombe
Frank A. Mugogo 116

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Yahitimisha Ziara ya Ukaguzi wa Miradi ya Umeme Mkoani Njombe

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imekamilisha ziara yake ya siku tatu mkoani Njombe kwa kukagua utekelezaji wa miradi ya Nishati Vijijini (REA) inayotekelezwa na serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO). Kwa upande wa REA ziara hiyo imehitimishwa katika kijiji cha Welela, Jimbo la Lupembe, ambapo kamati hiyo imepongeza juhudi zinazofanywa na Serikali kuhakikisha umeme unawafikia wananchi wa vijijini kwa kasi inayostahili.

Akizungumza wakati wa hitimisho la ziara hiyo, Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. David Mathayo, alisema kamati yake imeridhishwa na utekelezaji wa miradi hiyo, lakini akasisitiza kuwa bado kuna haja ya kuongeza kasi ili kufanikisha lengo la Serikali la kuhakikisha vitongoji vyote nchini vinaunganishwa na gridi ya taifa kwa wakati.

"Tumetembelea vijiji mbalimbali, vikiwemo Mang’oto, Lwangu na Welela, tumeona maendeleo mazuri ya usambazaji wa umeme wa REA. Hata hivyo, bado tunasisitiza kuongeza kasi ya utekelezaji ili wananchi wote wanufaike na huduma hii muhimu," alisema Dkt. Mathayo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, aliwahakikishia wananchi kuwa Serikali imejipanga kuhakikisha changamoto zote za umeme vijijini zinatatuliwa kwa haraka ili kuboresha maisha ya wananchi.

"Serikali inatambua umuhimu wa umeme kwa maendeleo ya wananchi, hususan katika sekta za elimu, afya, na biashara. Tutaendelea kuweka msukumo ili kuhakikisha vitongoji vyote vinapata umeme kwa wakati, na kwa hivyo kuchochea ukuaji wa uchumi wa wananchi," alisema Mhe. Kapinga.

Wananchi wa Kijiji cha Welela, Jimbo la Lupembe, wameeleza furaha yao kwa kupatiwa umeme kupitia Miradi ya umeme Vijijini inayoendelea kutekelezwa na REA, wakisema kuwa hatua hiyo imewasaidia kuondokana na changamoto ya kutembea umbali mrefu kutafuta huduma muhimu, ikiwemo mashine za kusaga nafaka.

Wakizungumza mbele ya Kamati ya Bunge, wananchi hao walieleza kuwa umeme huo umeleta mabadiliko makubwa katika maisha yao ikiwa ni pamoja na kuwaongezea kipato kwakua wanautumia kwa shughuli za kiuchumi.

Mmoja wa wakazi wa kijiji hicho, Oliva Kaduma, alisema kuwa uwepo wa umeme umeimarisha upatikanaji wa huduma za kijamii kwa urahisi, hali inayochochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika eneo hilo.

Kwa upande wake, Diwani wa Viti Maalumu wa Kata ya Mtwango, Rhoda Wanderage, aliishukuru Serikali kwa kuhakikisha upatikanaji wa umeme wa uhakika, akisema kuwa hatua hiyo imesaidia kutatua changamoto nyingi za kijamii na kiuchumi kwa wakazi wa eneo hilo. Pia, alitoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo inayowanufaisha wananchi wa vijijini.

"Zamani tulilazimika kutembea umbali mrefu kusaga nafaka au kupata huduma nyingine zinazotegemea umeme, lakini sasa kila kitu kipo karibu. Tunamshukuru sana Rais Samia kwa juhudi hizi," alisema Wanderage.

Naye Mkurugenzi wa umeme Vijijini kutoka wakala wa Nishati vijijini (REA), Mhandisi Jones Olotu, alieleza kuwa jumla ya shilingi bilioni 81.6  zinatumika kutekeleza miradi ya usambazaji wa umeme vijijini mkoani Njombe. Alibainisha kuwa miradi hiyo ni sehemu ya mpango wa kitaifa wa kuhakikisha vijiji vyote vinaunganishwa na gridi ya taifa, huku sehemu kubwa ya miradi hiyo ikiwa imekamilika ndani ya muda uliopangwa.

"Tunahakikisha kuwa vitongoji vyote vilivyoainishwa vinapata umeme kwa wakati. Pia, tupo katika hatua za mwisho za kutangaza Zabuni mpya ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya umeme vitongojini," alisema Mhandisi Olotu.

Ziara hiyo kwa upande miradi ya REA imehitimishwa kwa Kamati ya Bunge kupokea taarifa rasmi ya utekelezaji wa miradi ya umeme mkoani Njombe ambapo miradi inayotekelezwa na REA Mkoani Njombe inagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 81.6

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«July 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
30
REA Yasambaza Mitungi na Majiko ya Gesi kwa Watumishi wa Gereza la Ukonga Dar es Salaam

REA Yasambaza Mitungi na Majiko ya Gesi kwa Watumishi wa Gereza la Ukonga Dar es Salaam

Serikali imesambaza kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza (Gereza la Ukonga) mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na majiko yake 464 ili kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia kama njia ya utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya kupikia nchini ambapo msisitizo ni angalau asilimia 80 ya Watanzania wawe wanatumia Nishati Safi ifikapo Mwaka 2034.

Read more
1
Mhe. Rais Samia Apongezwa Kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Vitendo

Mhe. Rais Samia Apongezwa Kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia kwa Vitendo

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amepongezwa kwa kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia kwa vitendo.

Read more
2
REA Yasambaza Mitungi, Majiko ya Gesi kwa Watumishi 461 wa Magereza Mkoa wa Mara

REA Yasambaza Mitungi, Majiko ya Gesi kwa Watumishi 461 wa Magereza Mkoa wa Mara

Katika kuendelea kutekeleza Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imegawa jumla ya mitungi ya gesi ya kilogramu 15 pamoja na majiko ya sahani mbili 461 kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mara.

Read more
3
REA Yaja na Mpango Kabambe wa Kuwezesha Ujenzi wa Vituo vya Mafuta Vijijini

REA Yaja na Mpango Kabambe wa Kuwezesha Ujenzi wa Vituo vya Mafuta Vijijini

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mpango wa kuwezesha ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu vya bidhaa za mafuta (petrol na dizeli) maeneo ya vijijini ili kuondoa madhara yatokanayo na njia zisizo salama.

Read more
4
Watanzania Watakiwa Kuachana na Dhana Potofu Kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni Gharama

Watanzania Watakiwa Kuachana na Dhana Potofu Kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni Gharama

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umewasihi Watanzania kote nchini kuachana na dhana ya kwamba Nishati Safi ya Kupikia ni gharama ikilinganishwa na matumizi ya kuni na mkaa.

Read more
5
Vitongoji Vyote 64,359 Vitakuwa na Umeme Ifikapo 2030

Vitongoji Vyote 64,359 Vitakuwa na Umeme Ifikapo 2030

Imeelezwa kuwa hadi kufikia mwaka 2030 vitongoji vyote Tanzania Bara vitakuwa vimefikishiwa nishati ya umeme kupitia miradi mbalimbali inayotekelezwa na kusimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Read more
6
78
REA Yajizatiti Kufikisha Lengo la Taifa Kwenye Nishati Safi ya Kupikia

REA Yajizatiti Kufikisha Lengo la Taifa Kwenye Nishati Safi ya Kupikia

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Saidy amesema Wakala umejizatiti kuhakikisha 80% ya Watanzania wanatumia Nishati Safi ya Kupikia ifikapo mwaka 2034 kama ilivyoelekezwa katika Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia.

Read more
910111213
14151617181920
21222324252627
28293031123
45678910

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top