Wajumbe wa Menejimenti wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) wamekula kiapo cha Uadilifu wa Uongozi wa Umma kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za Utumishi na Uongozi wa Umma.
Wamekula kiapo hicho Jijini Dodoma Machi 11, 2025 mbele ya Afisa Maadili Sekretarieti ya Maadili ya Utumishi wa Umma, Kanda ya Kati, Bi Deborah Mwanjali katika Ofisi za REA.
Akifafanua lengo la kiapo hicho, Mwanjali amesema ni kuhakikisha kiongozi wa watumishi wa umma anakiri kwa dhamira yake kuishi katika mienendo ya kiuadilifu katika utumishi wa umma kama sheria zinavyomtaka.
Alisema kiapo hicho hufanyika pale kiongozi anapoteuliwa katika nafasi mpya, kiongozi anapohama kutoka taasisi moja kwenda nyingine.
Imetolewa na:
Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma