Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Kamati ya PAC Yaipongeza REA Usambazaji Umeme Katika Vijiji vya Mkoa wa Singida
Frank A. Mugogo 61

Kamati ya PAC Yaipongeza REA Usambazaji Umeme Katika Vijiji vya Mkoa wa Singida

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) chini ya Kaimu Mwenyekiti wake, Mhe. Joseph Kakunda leo, tarehe 14 Machi, 2025 imetembelea  na kukagua utekelezaji wa Miradi ya kusambaza  umeme vijijini mkoani Singida kupitia Miradi ya awali kama vile REA Awamu ya Kwanza (REA I), REA Awamu ya Pili (REA II), REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza (REA III Round I), na REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili (REA III Round II); ambapo vijiji vyote 441 vya mkoa huo vimefikiwa na umeme huku vitongoji 1,052 vimefikiwa na huduma ya umeme kati ya vitongoji 2,289 vya mkoa wa Singida, sawa na asilimia 45.96 ya vitongoji vyote.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya PAC, Mhe. Kakunda ameipongeza Bodi ya Nishati Vijijini (REB); Menejimenti ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Serikali kwa ujumla kwa kubuni, kuanzisha na kutekeleza Miradi mbalimbali ya kusambaza nishati ya umeme kwa Wananchi wa mkoa wa Singida na kuongeza kuwa umeme ni fursa ya kuboresha maisha ya Watu vijijini kama utatumika ipasavyo.

“Tumefurahishwa na tuliyoyaona hapa katika kijiji cha Kitopeni; Aghondi na kwenye zahanati ya kijiji cha Mabondeni. Tunaishukuru Serikali kupitia REA kwa udhibitisho wa uwepo wa umeme. Tunatoa wito kwa Wananchi, kasi ya kujiunganisha na huduma ya umeme, iongezeke; wekeni mpango ili kuhakikisha umeme unawasaidia kujiletea maendeleo yenu.” Amesema, Makamu Mwenyekiti wa PAC, Mhe. Kakunda.

Katika taarifa yake mbele ya Kamati ya PAC; Mkurugenzi wa Mipango na Utafiti Bwana Godfrey Chibulunje ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa REA; amesema Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini imetoa jumla ya shilingi bilioni 86.8 ili kuhakikisha Miradi minne (4) inatekelezwa mkoani humo ili kuhakikisha Wananchi wanafikiwa na huduma ya umeme ili kuwapa maendeleo ya kiuchumi na kijamii. 

“Wakala wa Nishati Vijijni (REA) unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali pamoja na kuwasimamia kwa karibu wakandarasi wote waliopewa zabuni ya kutekeleza miradi mbalimbali kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kwa ubora uliopangwa ili iweze kuwanufaisha Wananchi.”amesema Bwana Godfrey Chibulunje.

Kamati ya PAC ipo katika ziara ya ukaguzi wa miradi ya Maendeleo ambapo inatarajia kufanya ziara hiyo katika mkoa wa Singida, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Dar es Salaam.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«April 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
311234
CALL FOR PROPOSAL - Supply and Installation of Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions

CALL FOR PROPOSAL - Supply and Installation of Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions

The Rural Energy Agency issue the Second Call for applications from qualified suppliers to Supply and install Clean Cooking Solutions to Households, Public and Private Institutions through on-call basis.

Read more
56
789
Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24

Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24

Please find the attached Sector Performance Reports for Financial Year 2023-24:

Read more
10111213
14
Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania Kuboresha Maisha ya Wananchi

Wabia wa Maendeleo Waahidi Kuendelea Kushirikiana na Serikali ya Tanzania Kuboresha Maisha ya Wananchi

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego amuopengeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kazi kubwa ya kufikisha umeme vijijini hali iliyobadili maisha ya wananchi vijijini.

Read more
151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top