United States President, Barack Obama has urged the Tanzanian government to ensure effective implementation of the electricity projects under the multi-billion dollar ‘Power Africa project’, financed by the US. President Obama made the statement during a brief visit to the Symbion Power Plant in Ubungo, Dar es Salaam early July, this year, where he launched the project.
Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, ametaja miradi ya kipaumbele itakayotoa matokeo ya haraka ifikapo 2015/2016, na kunufaisha wananchi katika mikoa mbalimbali nchini. Prof. Muhongo aliitaja miradi hiyo mikubwa jijini Dar es Salaam mbele ya wadau waliokusanyika katika kongamano la wazi la siku moja kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.
Serikali imesema ipo tayari kushirikiana na Ujerumani katika kuzalisha umeme vijijini kwa kutumia nishati mbadala hususan upepo na jua. Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Profesa Sospeter Muhongo alipokutana na Ujumbe wa Wabunge kutoka Ujerumani.
Serikali ya Tanzania imekamilisha makubaliano ya fedha za msaada wa Krona milioni 700, sawa na shilingi bilioni 200 za Tanzania, kutoka Serikali ya Norway, kwa ajili ya kupeleka umeme vijijini. Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo alisaini mkataba wenye makubaliano hayo, Aprili 9, 2013 Mjini Oslo Norway akiiwakilisha Serikali ya Tanzania, ambapo Serikali ya Norway iliwakilishwa na Waziri wake wa Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa, Bw. Heikki Holmas.