Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA yawapa tuzo wakandarasi waliofanya vizuri miradi ya Peri Urban III
Frank A. Mugogo 141

REA yawapa tuzo wakandarasi waliofanya vizuri miradi ya Peri Urban III

Wakala wa Nishati Vijijini (REA), leo tarehe 24 Agosti, 2024 imewapa tuzo na vyeti maalum Wakandarasi waliofanya vizuri kupitia Mradi wa Kupeleka Umeme maeneo ya Pembezoni mwa Miji Awamu ya Tatu (Peri Urban III) kote nchini ndani ya muda uliopangwa na kwa ubora unatakiwa.

Awali, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi, Hassan, Saidy alisema utendaji madhubuti (Performance) na kukamilisha Miradi ya PERI Urban III kwa wakati kumechangia Wakandarasi hao kupewa tuzo hizo.

“Kipekee, niwapongeze Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kwa kuwasimamia Wakandarasi wazawa kwenye Miradi ya PERI Urban III na kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati. Natambua kuwa ninyi ndio mlio kuwa Washauri Elekezi wa mradi huu, hivyo mnao mchango mkubwa katika mafanikio haya”. Amekaririwa Mhandisi Saidy.

Mhandisi Hassan Saidy amesema kuwa REA iliahidi kuwa kwa sasa, itaanza kuwatunuku tuzo na vyeti kwa Wakandarasi wanaofanya vizuri kwenye usambazaji wa nishati ya umeme vijijini.

“Tuliahidi na sasa tumetimiza, tumeona hii ni njia nzuri ya kuwafanya waongeze nguvu, kwenye utekelezaji wa Miradi ya usambazaji wa nishati ya umeme vijijini, wale wanaofanya vizuri basi tuwatambue”. Amesisitiza Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi, Hassan Saidy.

Naye, Mgeni Rasmi wa hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB) Mhe. Balozi na Meja Jenerali Mstaafu, Jacob Kingu amewapongeza Wakandarasi hao kwa kumaliza kwa wakati na kwa ubora. 

“Kumbukeni kuwa, juhudi zenu zina mchango mkubwa katika maendeleo ya taifa letu, na kwa hivyo, endeleeni kujitolea kwa moyo ili kuhakikisha miradi yote, mliyopewa inakamilika kwa wakati.” Amesisitiza, Mhe. Balozi Kingu.

Naye Mkurugenzi wa Umeme Vijijini (DRE) kutoka REA, Mhandisi, Jones Olotu amesema hafla ya kuwapa tuzo Wandarasi hao umelenga kuwakumbusha na kuhusu wajibu wao wakati wa utekelezaji wa miradi ya usambazaji wa nishati vijijini pamoja kutambua juhudi zao kwenye maendeleo ya Sekta ya Nishati nchini.

Wakandarasi waliofanya vizuri na kutunukiwa tuzo na vyeti ni pamoja na kampuni kwanza ni ya DIEYNEM Co Ltd, kampuni ya pili ni DERM Group (T) Ltd, kampuni ya tatu ni Central Electricals & Electronics International Ltd na kampuni ya nne ni OK Electrical & Electronics Services Ltd, kampuni zote hizo ni za Watanzania.

Maeneo ya utekelezaji wa Miradi ya Kupeleka Umeme maeneo ya Pembezoni mwa Miji Awamu ya Tatu (Peri Urban III) sambamba na Wakandarasi hao ni kama ifuatavyo:  - kampuni ya DIEYNEM Co Ltd (Lot 2, mkoani Kagera); kampuni ya DERM Group (T) Ltd (Lot 4, mkoa wa Mbeya & Lot 5, mkoa wa Mtwara); Central Electricals & Electronics International Ltd (Lot 6, mkoa wa Singida) na mwisho OK Electrical Services Ltd (Lot 7, mkoa wa Tabora na Lot 8, mkoa wa Tanga).

Naye Mwakilishi kutoka Bodi ya Usajili wa Wakandarasi (CRB); Mhandisi, Gloria Simbakali ameipongeza REA kwa kuwaalika ili kushiriki hafla hiyo lakini pia amepongeza kwa hatua ya utoaji wa tuzo kwa Wakandarasi waliofanya vizuri kwa jukumu moja wapo la CRB ni kuratibu zoezi la usimamizi pamoja na uwajibikaji (Performance) kwa Wakandarasi (Wanachama). 

Akiongea kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO); Mhandisi, Robert Semsela ameipongeza REA kwa kutekeleza na kuendelea kuwafikia Wananchi wengi kupitia Miradi mbalimbali ya kusambaza umeme vijijini na kuongeza kuwa lengo ni kuboresha maisha ya Watu wa vijijini.

Naye, Mhandisi, Ridhuan Mringo, Mwenyekiti wa DERM Group ameipongeza Serikali kupitia REA kwa kutenga fedha za kutosha kwenye miradi ya kusambaza umeme vijijini mkubwa.

“Tunaishukuru Serikali kwa kuwa tunalipwa katika muda muhafaka kwa kila madai yetu ambayo ni halali na yamekidhi vigezo”. Alikaririwa, Mhandisi, Mringo.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«January 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
678
Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini Mkoani Lindi.

Read more
9101112
13141516171819
20212223242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top