Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Vijiji 151 Vimebaki Nchi Nzima Kupata Huduma ya Umeme – Kapinga
Aodax K. Nshala 91

Vijiji 151 Vimebaki Nchi Nzima Kupata Huduma ya Umeme – Kapinga

Kati ya Zaidi ya Vijivi 12,000 Nchi Nzima

Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Judith Kapinga amesema Vijiji 151 tu nchi nzima ndio ambavyo bado havijafikiwa na huduma ya umeme kati ya Vijiji zaidi ya 12,000 ambapo wilayani Ludewa mkoani Njombe vimebaki Vijiji nane.

Mhe. Kapinga ameyasema hayo jana tarehe 19 Julai 2024 wakati wa ziara ya kikazi katika Vijiji vya Lubonde na Maweni wilayani Ludewa mkoani Njombe akikagua miradi ya nishati.

Wakati wa ziara hiyo Mhe. Kapinga alifanikisha kuingiwa makubaliano kati ya Kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya Madope iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ya kukabidhi miundombinu ya kusafirisha na kusambaza umeme kwa Shirika hilo baada ya kusainiwa kwa mkataba kati ya pande hizo mbili.

Mhe. Kapinga amesema kuwa Serikali inathamini kazi kubwa inayofanywa na Kanisa Katoliki kwa kushirikiana na Serikali kwenye uwekezaji katika sekta mbalimbali.

Kwa upande wake Askofu wa jimbo la Njombe Eusebio Kyando ameupongezi Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ushirikiano wao na kutoa fedha zilizowezesha kufanikisha mradi huo.

Kampuni ya Madope ni miongoni mwa wazalishaji wadogo wa umeme katika Wilaya ya Ludewa ambayo inamilikiwa kwa asilimia 55 na Kanisa Katoliki jimbo la Njombe.

Share

Print
«January 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
678
Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini Mkoani Lindi.

Read more
9101112
13141516171819
20212223242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top