Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Ziara Bodi ya Nishati Vijijini Kigoma
Frank A. Mugogo 394

Ziara Bodi ya Nishati Vijijini Kigoma

REA Yatumia Zaidi ya Bilioni 100 Kutekeleza Miradi ya Umeme Vijijini Kigoma

Katika kuendelea kuboresha maisha ya wananchi Vijijini, Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umetumia zaidi ya Shilingi Bilioni 100 kutekeleza miradi ya kupeleka umeme vijijini katika Mkoa wa Kigoma.

Hayo yamebainishwa leo Septemba 18 Mkoani Kigoma wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Meja Jenerali (mstaafu), Jacob Kingu wakati wa ziara ya Bodi hiyo kukagua utekelezwaji wa miradi mbalimbali ya kupeleka umeme vijijini.

Wakati wa ziara hiyo, Mwenyekiti Kingu amewataka wakandarasi kuhakikisha wanamaliza miradi hiyo kwa wakati uliopangwa, na kwamba hawatasita kuwachukulia hatua za kimkataba mkandarasi yoyote atakayeshindwa kukamilisha miradi hiyo kwa wakati kama ilivyopangwa.

“Tumeshatoa maelekezo. Hakuna muda wa nyongeza utakaotolewa kwa mkandarasi atakayeshindwa kutekeleza mradi wake ndani ya muda uliopangwa, labda kwa sababu maalum. 

Tumewaelekeza wakandarasi pia wahakikishe material yote yanayohitajika kama nguzo kabla ya msimu wa mvua kuanza ili miradi hiyo isichelewe kama ilivyo dhamira ya serikali umeme kuwafikia wananchi wote ndani ya muda,” amesisitiza Mwenyekiti Kingu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Mhe. Balozi Radhia Msuya amesema kuwa ziara hiyo ni muendelezo wa ziara za Bodi hiyo kuhakikisha inatembelea miradi inayosimamiwa na REA kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati na kubadilisha hali za wananchi wa vijijini kama ilivyo adhma ya serikali.

Akizungumza awali, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy amesema kuwa katika mkoa wa Kigoma, jumla ya Vijiji 279 kati ya Vijiji 306 katika Mkoa wa Kigoma tayari vimeunganishwa na nishati ya umeme na kusisitiza kuwa safari ya kupeleka umeme katika Vitongoji imeanza.

“Zaidi ya vitongoji 595 wakandarasi wanaendelea na utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme. Katika vitongoji 1849 katika Mkoa wa Kigoma, vitongoji Zaidi ya 1370 tayari vimeshapata umeme. Tunaendelea kuhamasisha wananchi kuendelea kutumia miradi hii kutekeleza na kubuni shughuli za kiuchumi zitakazoweza kuboresha uchumi wao pamoja na kulinda miradi hii maana serikali imewekeza fedha nyingi sana,” amesema Mhandisi Saidy.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«January 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
2930311234
5678910
Wananchi Kahama Wamshukuru Rais Samia Kuwafikishia Umeme wa REA

Wananchi Kahama Wamshukuru Rais Samia Kuwafikishia Umeme wa REA

Wananchi Kata za Wendele na Mwendakulima Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga wamemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwawezesha kubadilisha maisha yao kupitia mradi wa umeme uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Read more
11
12131415
Serikali Kupitia REA Kuzindua Miradi Mikubwa Ya Kimkakati

Serikali Kupitia REA Kuzindua Miradi Mikubwa Ya Kimkakati

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatarajia kuzindua Kituo cha Kupoza na Kusambaza Umeme cha Mtera na Kusaini Mikataba ya kutekeleza mradi kabambe wa kusambaza umeme kwenye vitongoji 9,009 katika Mikoa yote Tanzania Bara.

Read more
161718
19
Mkurugenzi Mkuu REA Awafunda Wahandisi wa Mikoa

Mkurugenzi Mkuu REA Awafunda Wahandisi wa Mikoa

Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mha. Hassan Saidy amewaelekeza Wasimamizi wa Miradi wa Mikoa kuhakikisha wanaimarisha Mawasiliano na Ushirikiano na wadau mbalimbali kwenye maeneo ya miradi ili kurahisisha utekelezaji wake.

Read more
202122232425
2627
Rais Samia Apeleka Neema ya Umeme Katika Vitongoji Lindi

Rais Samia Apeleka Neema ya Umeme Katika Vitongoji Lindi

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inatekeleza mradi wa shilingi bilioni 25.8 wa kusambaza umeme katika vitongoji 159 utakaonufaisha kaya 5,116 Mkoani Lindi.

Read more
282930311
2345678

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top