Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani
Mohamed Saif 129

REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

Kwa sasa REA imetenga Bilioni 3 kuunganisha Kaya 803 na Taasisi Tatu Mkoa wa Pwani

Wakala Wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kufadhili miradi ya usambazaji wa gesi asilia kwa lengo la kuhakikisha kaya na taasisi za umma zinanufaika na matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, hatua inayochangia kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi na salama.

Akizungumza katika banda la REA Oktoba 28, 2026 wakati wa maonesho ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati, Mhandisi wa Miradi wa wakala, Mha. Ramadhani Mganga, amesema REA imetumia takribani shilingi bilioni 6.8 kuunganisha kaya 1,001 katika mikoa ya Lindi na Pwani kutumia nishati ya gesi asilia kupikia.

Amesema kati ya kaya hizo, 471 zipo mkoani Lindi, huku nyingine 530 zikiwa katika Kata ya Kisemvule, mkoani Pwani.

Mhandisi Mganga ameongeza kuwa REA imetenga takribani shilingi bilioni tatu kwa ajili ya kupanua huduma hiyo katika maeneo ambayo bado hayajafikiwa, hususan Kata ya Kisemvule, ambapo kaya nyingine 803 pamoja na shule tatu zinatarajiwa kuunganishwa na kunufaika na matumizi ya gesi asilia.

Amesisitiza kuwa uwekezaji huo unaonesha mchango wa REA katika kuhakikisha rasilimali ya gesi asilia inawanufaisha wananchi moja kwa moja kupitia upatikanaji wa nishati safi ya kupikia, sambamba na juhudi za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati hiyo nchini.

Maelezo hayo yametolewa wakati wa hafla ya utiaji saini leseni za utafutaji wa mafuta na gesi asilia katika vitalu vya Mnazi Bay North, Mnazi Bay West, Songosongo na Eyasi Wembere, vilivyopo katika maeneo ya kusini mwa Tanzania.

Hafla hiyo imeshuhudiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Deogratius Ndejembi, ambaye alikuwa mgeni rasmi.

REA imesisitiza kuwa kulingana na upatikanaji wa fedha itaendelea kushirikiana na wadau wa sekta ya nishati kufadhili miradi ya kuunganisha kaya na taasisi na huduma ya gesi asilia, ili wananchi wengi zaidi wanufaike na nishati safi, salama na rafiki kwa mazingira.

Share

Print
«November 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
26
REA, Benki Ya Dunia Wapeleka Tabasamu Kwa Wananchi Waishio Visiwani

REA, Benki Ya Dunia Wapeleka Tabasamu Kwa Wananchi Waishio Visiwani

Wananchi wanaoishi katika Visiwa wameipongeza na kuishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuwafikishia mifumo ya umeme jua kwa bei ya ruzuku hali iliyosaidia kuboresha maisha yao visiwani.

Pongezi hizo zimetolewa leo na wananchi wanaoishi katika Kisiwa cha Bezi kilichopo katika Wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ilipotembelea kisiwani hapo kuona maendeleo ya mradi huo ambao unafadhiliwa na benki hiyo na kusimamiwa na REA katika visiwa 120 nchini.

Read more
2728
REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kufadhili miradi ya usambazaji wa gesi asilia kwa lengo la kuhakikisha kaya na taasisi za umma zinanufaika na matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, hatua inayochangia kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi na salama.

Read more
2930
Miradi Ya Umeme Vijijini Imeboresha Huduma Za Kijamii - Ujumbe Benki ya Dunia

Miradi Ya Umeme Vijijini Imeboresha Huduma Za Kijamii - Ujumbe Benki ya Dunia

Benki ya Dunia yapongeza miradi ya umeme vijijini kwa kuboresha maisha ya wananchi vijijini pamoja na huduma za kijamii.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mtaalam Mwandamizi wa Fedha kutoka Benki ya Dunia, Nkundwe Mwakiluma wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Benki ya Dunia iliyolenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo na kusimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Read more
311
23
The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey

The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey

The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey provides data to inform energy-related programs and projects.

Read more
45678
9
Wizara Ya Maji, Nishati Na Madini Zanzibar Yatembelea REA Kujifunza Utekelezaji Wa Miradi Ya Nishati Safi Ya Kupikia

Wizara Ya Maji, Nishati Na Madini Zanzibar Yatembelea REA Kujifunza Utekelezaji Wa Miradi Ya Nishati Safi Ya Kupikia

Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar (MOWEM), imetembelea Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034).

Read more
10
REA Yaahidi Ushirikiano, Katika Utekelezaji Wa Mkakati Wa Nishati Safi Ya Kupikia Zanzibar

REA Yaahidi Ushirikiano, Katika Utekelezaji Wa Mkakati Wa Nishati Safi Ya Kupikia Zanzibar

Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar (MOWEM) imekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy yaliyolenga kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024–2034).

Read more
1112131415
16171819202122
23242526272829
30123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top