Mkuu wa Wilaya ya Ludewa Mhe. Olivanus Thomas akimwakilisha Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhe. Anthony Mtaka leo Oktoba 20,2025 amezindua rasmi mradi wa usambazaji na uuzaji wa majiko banifu kwa bei ya ruzuku mkoa wa Njombe. uzinduzi huo umeongozwa na mkuu wa wilaya, Maafisa kutoka REA pamoja na viongozi wengine wa mkoa, wilaya, kata, vijiji na vitongoji vyake.