Bodi ya Nishati Vijijini (REB) katika kikao kilichofanyika Desemba 20, 2020 imemteua Mhandisi Amos William Maganga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuanzia tarehe 16 Desemba 2020 kwa mujibu wa kifungu cha 25(1) cha Sheria Namba 8 ya Nishati Vijijini ya Mwaka 2005.
Norway, Sweden and European Union announce a contribution for a total amount of 142 TZS Billion (USD 61 million) to “the Densification Round 2A Project” as part of the Government of Tanzania’s Rural Electrification Programme – Turnkey III, running until the end of 2021.
Serikali inafanya Utafiti wa Hali ya Upatikanaji na Matumizi ya Umeme Tanzania Bara kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) pamoja na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (National Bureau of Statistics) Mwaka 2019-2020.
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unatoa ufafanuzi kuhusu habari iliyochapishwa katika gazeti la Jamhuri Toleo Na. 295 la tarehe 23 – 29 Mei, 2017 yenye kichwa cha habari “ Waziri apiga dili” ununuzi wa zabuni ya wakandarasi wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu kwamba ulizingatia Sheria ya Ununuzi wa Umma ya Mwaka 2011 (kama ilivyofanyiwa marekebisho Mwaka 2016) pamoja na kanuni zake.
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umekamilisha taratibu za zabuni kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu (Turnkey III) na unawajulisha Wakandarasi walioshinda kwamba hatua inayofuata ni kupewa barua za tuzo (Award Letters) na kusaini mikataba.
Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), imeanza utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Awamu ya Tatu utakaojumuisha vijiji 7,873 katika wilaya na mikoa yote ya Tanzania Bara. Kati ya vijiji hivyo, vijiji 7,697 vitapelekewa umeme wa gridi na vijiji 176 umeme wa nje ya gridi (off-grid).
Wakala wa Nishati Vijijini unatoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa zilizoandikwa kwenye magazeti ya Jambo Leo na Mwanahalisi ya Ijumaa Tarehe 15 Aprili 2016 pamoja na Gazeti la Habari Leo la Jumamosi Tarehe 16 Aprili 2016.
Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (MB) ameandaa kikao cha siku tatu kwa ajili ya kukutana na wakandarasi wakubwa (Main Contractors) na wakandarasi wadogo (Sub-Contractors) wanaotekeleza miradi ya kusambaza umeme vijijini Awamu ya Pili tarehe 29 hadi 31 Machi, 2016.