Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imefanya ziara ya siku moja katika Mradi wa Umeme wa Julius Nyerere uliopo Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo ambao ukikamilika utawezesha upatikanaji wa umeme wa uhakika nchini.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt Merdad Kalemani amezindua Mradi wa Ujazilizi Fungu la Pili tarehe 24 Septemba 2020. Mradi huu unalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vitongoji katika vijiji vilivyofikiwa na miundombinu ya umeme.
Bodi ya Nishati Vijijini (REB) haijaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa kusambaza umeme vijijini katika Wilaya ya Iramba na Mkalama mkoani Singida unayotekelezwa na Kampuni ya Emerc and Dynamic Engineering.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo amekipongeza kikosi cha Suma JKT ambacho kimepewa kazi kujenga miundombinu ya kusambaza umeme katika kata ya Kwa Mtoro na Farkwa.
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeibuka na ushindi wa pili katika kundi la Wakala wa Serikali katika Maonesho ya Nanenane yanayofanyika kitaifa katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo ametoa wito kwa viongozi na watendaji wa vijiji kulinda miundombinu ya usambazaji wa umeme katika vijiji vyao ili kuepusha hasara ambayo Serikali inapata kutokana na uharibifu wa miundombinu hiyo.
WAZIRI WA NISHATI MHE. DKT. MEDARD MATOGOLO CHANANJA KALEMANI (MB.) AMEWASILISHA BUNGENI LEO, TAREHE 08 MEI, 2020 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2020/21
Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaunga mkono juhudi za Serikali za kuchukua tahadhari dhidi ya kuenea kwa maambukizi ya ugonjwa wa homa kali ya mapafu (COVID-19) inayosababishwa na virusi vya corona. Tunawaomba wadau wetu wote kushiriki pamoja katika mapambano haya.