Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani ameagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme (TANESCO) kuweka mpango ambao utawezesha vifaa vyote vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme vinatengenezwa hapa nchini.
Uploaded is the REPDF Lot 1 Consultant Database.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dr. John Pombe Magufuli amemteua Wakili Julius B. Kalolo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakala wa Nishati Vijijini.
Bodi ya Wakurugenzi ya Wakala wa Nishati Vijijini imekutana wa Wakandarasi wa Mradi wa REA Awamu ya III Mzunguko wa I katika Ukumbi wa Hazina, Dodoma kujadili changamoto mbalimbali zinazoweza kuchelewesha utekelezaji wa Mradi.
WAZIRI WA NISHATI MHE. DKT. MEDARD MATOGOLO CHANANJA KALEMANI (MB.) AMEWASILISHA BUNGENI LEO, TAREHE 28 MEI, 2019 MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA NISHATI KWA MWAKA 2019/20
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, tarehe 06/04/2019 amezindua Mradi wa kusafirisha umeme wa kilovolti 220 kutoka Makambako hadi Songea. Jumla ya wateja wa awali 22,700 wanatarajiwa kuunganishiwa na huduma ya umeme kupitia Mradi huu kwenye vijiji 122.
Balozi wa Norway nchini Tanzania, Ms. Elisabeth Jacobsen ametembelea Ofisi za Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kufanya mazungumzo na Menejimenti ya Wakala tarehe 28 Februari, 2019.
Waziri wa Nishati, Mh. Dk. Medard Kalemani amezindua Bodi ya Nishati Vijijini (REB), leo tarehe 18 Februari, 2019 itakayosimamia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutoa maelekezo mbalimbali yatakayopelekea kazi ya usambazaji umeme vijijini kufanyika kwa kasi na ufanisi.