Monday, February 18, 2019 Admin.Frank Mugogo 12486 News, Announcements, Tenders UTEUZI WA WAJUMBE WA BODI MPYA YA NISHATI VIJIJINI (REB) Waziri wa Nishati, Mh. Dk. Medard Kalemani amezindua Bodi ya Nishati Vijijini (REB), leo tarehe 18 Februari, 2019 itakayosimamia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kutoa maelekezo mbalimbali yatakayopelekea kazi ya usambazaji umeme vijijini kufanyika kwa kasi na ufanisi..Uzinduzi wa Bodi hiyo umefanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wizara ya Nishati akiwemo Naibu Waziri wa Nishati, Mh. Subira Mgalu; Katibu Mkuu, Dkt. Hamisi Mwinyimvua; Kaimu Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga; Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Raphael Nombo; Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Amos Maganga na watendaji wengine kutoka Wizara na Wakala wa Nishati Vijijini.Mh. Waziri wa Nishati alieleza kuwa, Bodi mpya ya Nishati Vijijini imeundwa kufuatia kuvunjwa kwa Bodi iliyopita tarehe 12 Novemba, 2018 kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushindwa kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kushindwa kusimamia vizuri Wakala wa Nishati Vijijini.Wajumbe wapya wa Bodi hiyo ni kama ifuatavyo:Dr. Andrew Marceline Komba - MjumbeMs. Dailin Leonard Mgweno - MjumbeMr. Oswald Martin Urasa - MjumbeMr. Henry Mwatwinzwa Mwimbe - MjumbeEng. Styden Rwebangira - MjumbeMr. Louis Passian Accaro - MjumbeMr. Francis M. Songela - MjumbeMkurugenzi MkuuWakala wa Nishati Vijijini (REA)Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2Barabara ya Sam NujomaS. L. P 7990Dar es Salaam, TanzaniaBarua Pepe: info@rea.go.tzSimu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003Nukushi: +255 22 2412007 Tags Announcements Business News Share Print Switch article Report for Evaluation of REA Funded Projects Previous Article BALOZI WA NORWAY ATEMBELEA OFISI ZA WAKALA WA NISHATI VIJIJINI (REA) Next Article