Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
Rais Samia Ashuhudia Tukio la Utiaji Saini Mikataba ya Umeme Vijijini na Uimarishaji Gridi
Veronica M. Simba 694

Rais Samia Ashuhudia Tukio la Utiaji Saini Mikataba ya Umeme Vijijini na Uimarishaji Gridi

Bilioni 385 zitatumika

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameshuhudia tukio kubwa la kihistoria la utiaji saini mikataba ya utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini pamoja na uimarishaji gridi ya Taifa.

Jumla ya mikataba 14 imesainiwa baina ya Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Kampuni mbalimbali za Wakandarasi ikihusisha miradi mitatu mikubwa.

Mradi wa kwanza ni kupeleka umeme kwenye vitongoji 1,522 katika mikoa 9. Wa pili ni kupeleka umeme katika maeneo 336 ya wachimbaji wadogo wa madini na wa tatu ni kupeleka umeme katika vituo vya afya, pampu za maji  399 pamoja na kuunganisha wateja wa awali 108,178.

Akizungumza katika hafla hiyo fupi iliyofanyika Februari 14, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia ameipongeza Wizara ya Nishati, REA na TANESCO kwa kazi waliyoifanya kuwezesha kufikia hatua hiyo ya utiaji saini mikataba ambayo alisema inalenga kuwanufaisha wananchi.

Rais Samia amebainisha kuwa matumaini yake ni kuona miradi husika ikienda kushamirisha uchumi na biashara kwa lengo la kuinua hali ya maisha ya wananchi.

“Huku ndiko kuwajali wanyonge, siyo kusimama kuwaongelea na kuzidi kuwatia unyonge. Tukipeleka umeme wa kutosha kwenye migodi, hali itabadilika kwani wataweza kutumia mitambo bora zaidi katika shughuli zao za uchimbaji na hivyo wataongeza mapato,” ameeleza Rais Samia.

Aidha, amefafanua kuwa umeme katika shughuli za kilimo utawezesha kufanya kilimo cha kibiashara ambacho kina manufaa zaidi kulinganisha na kilimo cha kawaida.

Vilevile, amesema umeme katika vituo vya afya utaboresha zaidi utoaji huduma kwa wananchi hususani kupunguza kwa kiasi kikubwa vifo vya akina mama na watoto, ambavyo kwa kiasi kikubwa husababishwa na mazingira duni ya kujifungulia akina mama wajawazito.

Halikadhalika, ameeleza kuwa umeme katika vyanzo vya maji utawezesha upatikanaji wa huduma hiyo kwa wingi na ubora zaidi.

Akizungumzia Mkakati wa Serikali kupeleka huduma za Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) maeneo ya vijijini, Rais Samia amesema ili kufanikisha Mpango huo, upelekaji umeme wa uhakika vijijini unatakiwa kwani pasipo nishati hiyo, mkakati husika hautafanikiwa.

Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Samia amewasisitiza Wakandarasi waliosaini mikataba kufanya kazi kwa bidii na kutimiza makubaliano yaliyofanyika. Amewaonya kuepukana na tamaa zinazoweza kusababisha utekelezaji duni wa kazi.

Pia, amekemea suala la wakandarasi wenye tabia ya kulalamika pale wanaposhindwa kukidhi vigezo na kukosa tenda hali inayowafanya kuzifuata Mamlaka mbalimbali ikiwemo PCCB na PPRA wakitaka ziingilie kati kwa kusimamisha mchakato husika au kuomba urudiwe ili wao wapate tenda hizo.

“Uteuzi wa Wakandarasi unafanywa kwa umakini mkubwa. Ili miradi hii itekelezwe haraka na tupate maendeleo ya haraka, tunahitaji maamuzi ya haraka. Wakandarasi mnaokosa tenda, mkianza kuzunguka PCCB ama PPRA mnazuia miradi na utekelezaji kwenda haraka,” amesisitiza.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, January Makamba amesema ifikapo Desemba mwaka huu (2023), kila kijiji Tanzania kitakuwa kimefikiwa na umeme.

Hata hivyo, ameeleza kuwa, kufikisha umeme vijiji vyote haimaanishi kuwa ni kusambaza umeme vitongoji vyote. “Unaweza ufikishe umeme vijiji vyote lakini ukawa hujavifikia vitongoji vyote, hivyo nakushukuru Mheshimiwa Rais kutoa maelekezo kuwasilishwa katika Baraza la Mawaziri Mpango wa kupeleka umeme vitongojini,” amebainisha.

Akizungumza zaidi, Waziri Makamba amesema kuwa serikali inatarajia kujenga mradi mkubwa wa umeme wa kuimarisha Gridi ya Taifa ambao utaigharimu serikali shilingi trilioni 4.42 ambao utakamilika ndani ya kipindi cha miaka minne.

Amesema katika mwaka huu wa fedha 2022/2023, serikali imetenga shilingi bilioni 500 ili kuanza utekelezaji wa mradi huo, ambao utakuwa ukitekelezwa kwa awamu tofauti.

“Kukamilika kwa mradi huo itakuwa ni historia kubwa kwa nchi yetu, hasa kwa vizazi vijavyo kuwa kuwa na umeme wa kutosha na wa uhakika.”

Alisema hadi kufikia mwaka 2025 Serikali inatarajia kufikisha megawati 5000 za umeme nchi nzima.

Akiwasilisha taarifa fupi ya Wakala kuhusu miradi iliyosainiwa, Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi Hassan Saidy alisema kwamba kwa kutambua umuhimu wa uwepo wa nishati bora na endelevu katika maeneo yote yakiwemo ya vijijini, Serikali kwa kushirikiana na Jumuia ya Ulaya na Ufaransa, imetoa Shilingi bilioni 385 ili kuwezesha utekelezaji wa miradi hiyo.

Akitoa takwimu, Mhandisi Saidy alieleza kuwa tangu kuanzishwa kwake mwaka 2007, REA imeweza kutekeleza miradi mbalimbali iliyochangia kufikisha huduma ya umeme katika vijiji 9,467 kati ya 12,345 vilivyopo Tanzania Bara sawa na asilimia 76.7  ikiwa ni takwimu za hadi mwezi Januari 2023.

Aidha, aliongeza kuwa vijiji 2,878 vilivyobaki, wakandarasi wanaendelea na shughuli za ujenzi wa miundombinu ya kupeleka umeme kupitia mradi unaoendelea wa REA Awamu ya Tatu Mzunguko wa Pili unaotarajiwa kukamilika Disemba mwaka huu wa 2023 na hivyo kufanya vijiji vyote kufikiwa na huduma ya umeme.

“Kwa upande wa vitongoji, kati ya vitongoji 64,760 vilivyopo nchini, vitongoji 28,424 sawa na asilimia 43.9 vilikwishafikiwa na huduma ya umeme. Serikali inaendelea na mipango ya kuongeza mafungu katika Mfuko wa Nishati Vijijini ili kuongeza kasi ya kufikisha umeme katika vitongoji 36,336 vilivyobaki,” alifafanua.

Kuhusu manufaa ya utekelezaji wa miradi ya nishati vijijini, Mhandisi Saidy alieleza kuwa ni pamoja na kuchangia ipasavyo katika ukuaji wa uchumi katika maeneo ya vijijini, kuboresha huduma za jamii vijijini zikiwemo afya, elimu, maji safi, mawasiliano na usalama pamoja na kuhifadhi mazingira na kuimarisha usalama.

Mkurugenzi Mkuu, kwa niaba ya Bodi ya Wakurugenzi na Watumishi wote wa Wakala, alimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuendelea kutoa fedha katika kutekeleza miradi ya kusambaza nishati vijijini akifafanua kuwa tangu Serikali ya Awamu ya Sita iingie madarakani, Wakala umesaini mikataba ya miradi mitano yenye thamani ya shilingi trilioni 1.7

“Pia Wakala unashukuru sana uungaji wako mkono kwa juhudi na mipango mizuri ya Mheshimiwa Waziri wa Nishati katika kuboresha na kuharakisha utolewaji na upatikanaji wa huduma za nishati ya umeme pamoja na nishati safi ya kupikia maeneo mbalimbali nchini,” alieleza Mhandisi Saidy.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na watu kutoka makundi mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, wataalamu wa sekta mbalimbali pamoja na wananchi.

Rate article

4.7
Rate this article:
4.7

Share

Print
«April 2024»
MonTueWedThuFriSatSun
25
Mkopo Nafuu wa Uwezeshaji wa  Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za  Mafuta (Petroli na Dizeli) Vijijini

Mkopo Nafuu wa Uwezeshaji wa Ujenzi na Uendeshaji wa Vituo Vidogo vya Bidhaa za Mafuta (Petroli na Dizeli) Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini unakaribisha maombi ya mkopo nafuu kuwezesha ujenzi wa vituo vidogo vya kuuzia bidhaa za mafuta (petroli na dizeli) vijijini. Mkopo huu utasaidia uwezeshaji wa ujenzi na uendeshaji wa vituo vipya vidogo vya gharama nafuu maeneo ya vijijini ili kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya mafuta kwa gharama nafuu, kwa njia salama, na isiyo na madhara kwa mazingira.

Wakala unawasisitiza waombaji walioomba katika awamu ya kwanza na kutokidhi vigezo kuomba tena baada ya kufanya marekebisho  ya  mapungufu yaliyobainishwa katika maombi yao. Aidha maombi mapya ya mkopo yanakaribishwa.

Read more
262728293031
12345
Call for Proposals for Results Based Financing (RBF) Application for Stand Alone Solar Home System (SA-SHS)

Call for Proposals for Results Based Financing (RBF) Application for Stand Alone Solar Home System (SA-SHS)

The Rural Energy Agency (REA) invites eligible firms to apply for grant per new SA-SHS installation in targeted rural communities. The grant includes end-user buying price system subsidization and firm’s performance incentive. The SA-SHS grant application is implemented through the program for Tanzania Rural Electrification Expansion Program Additional Financing (TREEP AF) which is supported by the World Bank.

Read more
67
891011121314
15
Wabia wa Maendeleo Waipongeza REA

Wabia wa Maendeleo Waipongeza REA


Wabia wa Maendeleo ambao wanafadhili miradi ya kusambaza nishati vijijini wamepongeza Wakala wa Nishati Vijijini kwa utekelezaji wa miradi ya kusambaza nishati vijijini ambayo inaleta tija kwa ustawi wa wananchi.

Read more
161718192021
22232425262728
293012345

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
PSSSF Building, 7th Floor
Makole Road
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top