Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA Yaanza Uhamasishaji Kwa Wananchi Kujiunga na Huduma ya Umeme Kwenye Vitongoji Mkoani Simiyu
Frank A. Mugogo 238

REA Yaanza Uhamasishaji Kwa Wananchi Kujiunga na Huduma ya Umeme Kwenye Vitongoji Mkoani Simiyu

Timu ya wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kushirikiana na timu ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tarehe 03 Oktoba, 2025 wameanza zoezi la uhamasishaji kwa Wananchi ili wajiunge na huduma ya umeme kwenye vitongoji mbalimbali vya mkoa wa Simiyu.

Akizungumza na Wanahabari, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka REA, Bi. Jaina Msuya amesema lengo la uhamasishaji huo ni kuongeza hamasa ya kujiunga na huduma ya umeme pamoja na kuongeza uelewa wa faida za matumizi ya nishati ya umeme ili Wananchi wa vijijini wabadili maisha yao kiuchumi na kijamii katika vitongoji vyao.

“Kujiunga na huduma ya umeme wakati mkandarasi akiwa yupo kwenye eneo la Mradi, ni nafuu kwa kuwa Mwananchi atalipia shilingi 27,000 kama gharama ya kujiunga na huduma hiyo ingawa kuna gharama ya kufanya ‘wiring’ na kama Mwananchi atakuwa hana fedha ya kufanya hivyo basi anaweza kununua kifaa maalum kinachitwa *Umeme Tayari* (UMETA) kwa gharama ya shilingi 36,000 tu,” amesema Bi. Jaina.

Kwa upande wake Mhandisi wa Miradi ya Umeme Vijijini mkoani Simiyu, Deusdedit Msanze amesema, uhamasishaji ni muhimu kwa sababu unawakumbusha Wananchi kujiunga na huduma ya umeme ndani ya muda mkandarasi anapokuwa bado yupo kwenye maeneo ya Miradi na kuchelewa kujiunga kunaongeza gharama kwa Wananchi.

Akiwahamasisha Wananchi wa Kitongoji cha Mwamahe, kijiji cha Ikinabushu, kilichopo katika Halmashauri ya wilaya ya Bariadi ambapo mkandarasi, kampuni ya Jiangsu Etern Co., Ltd kutoka China ameshakamilisha ujenzi wa miundombinu na Mradi utafungwa na kukabidhiwa kwa TANESCO, tarehe 15 Novemba, 2025 ambapo katika Wananchi 43 wanaostahili kujiunga na huduma ya umeme ni Wananchi saba (7) tu ndiyo waliojiunga na huduma hiyo.

Baada ya uhamasishaji huo Wananchi 20 walijaza fomu ya maombi ya kujiunga na huduma ya umeme ambapo zoezi hilo liliongozwa na Afisa Uhusiano na Wateja kutoka TANESCO mkoa wa Simiyu, Bwana Amon Bidebuye.

Bwana Amon amesema kila Mwananchi mwenye sifa ya kujiunga na huduma ya umeme anaweza kujaza fomu ya maombi kupitia simu ya aina yoyote (Simu Janja au Kiswaswadu) ili kuomba kuunganishwa na huduma ya umeme kwa kupiga *152*00# na baada ya hapo wanatakiwa wafuate maelekezo ambayo ni rahisi.

“Nitoe wito kwa Wananchi, ukitaka kuomba kujiunga na huduma ya umeme, haulazimiki kwenda ofisi ya TANESCO wilayani au mkoani, unaweza kuomba kujiunga kwa kutumia simu yako ya kiganjani na utatakiwa uwe na namba ya NIDA au na Kitambulisho cha NIDA.” amesisitiza Bwana Amon.

Zoezi la uhamaishaji linaendelea katika wilaya ya Itilima na Meatu na Maswa mkoani humo kwa kupitia mikutano kwa Wananchi pamoja na uhamasishaji wa nyumba kwa nyumba.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini
Jengo la REA
28 Mtaa wa Medeli
Dodoma

Share

Print
«December 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
242526
Rais Samia Atoa Ruzuku ya Kufanya  Wiring Miradi ya Umeme Vijijini

Rais Samia Atoa Ruzuku ya Kufanya Wiring Miradi ya Umeme Vijijini

Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaanza kutekeleza mradi wa kutandaza nyaya za umeme (wiring) kwa wananchi kupitia miradi ya kusambaza umeme inayotekelezwa na wakala kote nchini.

Read more
27282930
123
Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya Nishati Safi

Hafla ya Utiaji Saini Mikataba ya Nishati Safi

Karibu katika Hafla ya Kusaini Mikataba ya Kufunga Miundombinu ya Nishati Safi katika Shule za Sekondari 52 pamoja na Chuo cha VETA.

Read more
4567
891011121314
15161718192021
22232425262728
2930311234

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top