Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
REA YASHINDA TUZO ZA TAASISI BORA ZA UMMA DUNIANI
Iddy Mwema 1

REA YASHINDA TUZO ZA TAASISI BORA ZA UMMA DUNIANI

Yapongezwa Kwa Kuboresha Maisha ya Wananchi Vijijini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeibuka miongoni mwa washindi wa tuzo za Dunia za Utumishi wa Umma (World Public Service Awards, 2026), zilizolenga kutambua mchango wa Taasisi na Mashirika ya Umma  unaotokana na huduma zinazotolewa na namna  zinavyoboresha maisha ya wananchi kwa ujumla.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo zilizofanyika Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Dubai, Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala, Mhandisi, Advera Mwijage kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mhandisi, Hassan Saidy, amesema kuwa wamepokea kwa furaha tuzo hiyo na kwamba tuzo hiyo inakwenda kuwa chachu ya kufanya kazi kwa bidii ili kuendelea kuboresha maisha ya wananchi vijijini.

“Tuzo hii kwetu ina maana kubwa sana na imekuwa kama deni kwetu kwa kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi  kuhakikisha wananchi vijijini wanaendelea kupata nishati bora, salama, endelevu na nafuu kwa maendeleo yao na kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla,” amesema Mhandisi, Mwijage.

Mhandisi, Mwijage amesema kuwa mafanikio yaliyofikiwa yasingeweza kufikiwa kama Serikali isingetoa fedha kwa wakati kuwezesha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya nishati vijijini.

“Tungependa kuishukuru Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwa wakati pamoja na Wabia wa Maendeleo wanaoshirikiana na Serikali katika kufadhili miradi mbalimbali tunayotekeleza. Kwa pamoja tumeweza kuyagusa maisha ya wananchi vijijini na matokeo yake yamefanya tuweze kutambulika Kitaifa na Kimataifa kwa kupatiwa  tuzo mbalimbali ikiwamo tuzo hii,” ameongeza, Mhandisi Mwijage.

Ameongeza kuwa, REA itaendela kutekeleza na kubuni miradi inayolenga kuendelea kuboresha maisha ya wananchi vijijini kupitia sekta ya nishati.

Share

Print
«November 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
26
REA, Benki Ya Dunia Wapeleka Tabasamu Kwa Wananchi Waishio Visiwani

REA, Benki Ya Dunia Wapeleka Tabasamu Kwa Wananchi Waishio Visiwani

Wananchi wanaoishi katika Visiwa wameipongeza na kuishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa kuwafikishia mifumo ya umeme jua kwa bei ya ruzuku hali iliyosaidia kuboresha maisha yao visiwani.

Pongezi hizo zimetolewa leo na wananchi wanaoishi katika Kisiwa cha Bezi kilichopo katika Wilaya ya Ilemela, Mkoa wa Mwanza wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Benki ya Dunia ilipotembelea kisiwani hapo kuona maendeleo ya mradi huo ambao unafadhiliwa na benki hiyo na kusimamiwa na REA katika visiwa 120 nchini.

Read more
2728
REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

REA Yatumia Bilioni 6.8 Kuunganisha Kaya 1,001 Na Gesi Asilia Mikoa Ya Lindi Na Pwani

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kufadhili miradi ya usambazaji wa gesi asilia kwa lengo la kuhakikisha kaya na taasisi za umma zinanufaika na matumizi ya nishati safi na salama ya kupikia, hatua inayochangia kupunguza utegemezi wa nishati zisizo safi na salama.

Read more
2930
Miradi Ya Umeme Vijijini Imeboresha Huduma Za Kijamii - Ujumbe Benki ya Dunia

Miradi Ya Umeme Vijijini Imeboresha Huduma Za Kijamii - Ujumbe Benki ya Dunia

Benki ya Dunia yapongeza miradi ya umeme vijijini kwa kuboresha maisha ya wananchi vijijini pamoja na huduma za kijamii.

Pongezi hizo zimetolewa leo na Mtaalam Mwandamizi wa Fedha kutoka Benki ya Dunia, Nkundwe Mwakiluma wakati wa ziara ya Ujumbe kutoka Benki ya Dunia iliyolenga kukagua maendeleo ya utekelezaji wa miradi inayofadhiliwa na Benki hiyo na kusimamiwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Read more
311
23
The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey

The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey

The 2024/25 Energy Access and Use Situation Survey provides data to inform energy-related programs and projects.

Read more
45678
9
Wizara Ya Maji, Nishati Na Madini Zanzibar Yatembelea REA Kujifunza Utekelezaji Wa Miradi Ya Nishati Safi Ya Kupikia

Wizara Ya Maji, Nishati Na Madini Zanzibar Yatembelea REA Kujifunza Utekelezaji Wa Miradi Ya Nishati Safi Ya Kupikia

Timu ya Wataalam kutoka Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar (MOWEM), imetembelea Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa lengo la kujifunza na kubadilishana uzoefu wa utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024-2034).

Read more
10
REA Yaahidi Ushirikiano, Katika Utekelezaji Wa Mkakati Wa Nishati Safi Ya Kupikia Zanzibar

REA Yaahidi Ushirikiano, Katika Utekelezaji Wa Mkakati Wa Nishati Safi Ya Kupikia Zanzibar

Timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Nishati na Madini Zanzibar (MOWEM) imekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Mhandisi Hassan Saidy yaliyolenga kujifunza na kubadilishana uzoefu kuhusu utekelezaji wa Mkakati wa Taifa wa Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia (2024–2034).

Read more
1112131415
1617181920
REA Kuendelea Kuwezesha Sekta Binafsi Kushiriki Kuzalisha Umeme

REA Kuendelea Kuwezesha Sekta Binafsi Kushiriki Kuzalisha Umeme

Bodi ya Nishati Vijijini (REB) imeeleza kuridhishwa na maendeleo ya mradi wa ndogo wa uzalishaji wa umeme kwa kutumia mfumo wa umeme jua unaochangia Megawati Tano katika Gridi ya Taifa.

Akizungumza leo Novemba 19, 2026 wakati wa ziara ya kutembelea mradi huo katika Kijiji cha Bugando Wilayani Magu Mkoani Mwanza, Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini REB, Mhe. Balozi Radhia Msuya amesema kukamilika kwa mradi huo ni hatua muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi na maendeleo ya Wilaya ya Magu na Taifa kwa ujumla, huku akiahidi kuwa, REA itaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendeleza miradi ya kuzalisha umeme kwa njia mbalimbali inayobuniwa na kutekelezwa na waendelezaji wadogo.

Read more
2122
23242526272829
REA YASHINDA TUZO ZA TAASISI BORA ZA UMMA DUNIANI

REA YASHINDA TUZO ZA TAASISI BORA ZA UMMA DUNIANI

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeibuka miongoni mwa washindi wa tuzo za Dunia za Utumishi wa Umma (World Public Service Awards, 2026), zilizolenga kutambua mchango wa Taasisi na Mashirika ya Umma  unaotokana na huduma zinazotolewa na namna  zinavyoboresha maisha ya wananchi kwa ujumla.

Read more
30123456

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top