Saturday, April 15, 2017 Admin.Frank Mugogo 11367 News UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA MBEYA Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Mbeya. Mgeni rasmi Katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 20/03/2017 katika Kijiji cha Ilinga, Kata ya Ibigi, Wilaya ya Rungwe alikuwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo.Mradi huu unajumuisha vipengele-mradi vitatu vya Grid Extension, Densification ambayo inalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya vijiji na vitongoji havikuungwa. Kipengele-mradi cha tatu kinahusisha usambazaji wa nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi.Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Mbeya utahusisha vipengele vyote vitatu. Mradi huu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti. Sehemu ya awali itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 304 (vya Mikoa ya Mbeya na Songwe) kwa gharama ya Shilingi Bilioni 72.8. Utekelezaji wa sehemu hii ya kwanza umeanza Mwezi Februari 2017 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 2019.Aidha, sehemu ya pili ya mradi huu wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu itaanza kutekelezwa baada ya sehemu ya kwanza kukamilika Mwaka 2019 ambapo vijiji 92 vitapatiwa umeme na hivyo kufikisha umeme katika vijiji vyote vya Mikoa ya Mbeya na Songwe ifikapo Mwaka 2021.Imetolewa na:Mkurugenzi MkuuWakala wa Nishati Vijijini (REA)Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2Barabara ya Sam NujomaS. L. P 7990Dar es Salaam, TanzaniaBarua Pepe: info@rea.go.tzSimu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003Nukushi: +255 22 2412007 Tags News Share Print Switch article UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA MARA Previous Article UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA SHINYANGA Next Article