Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA SHINYANGA
Admin.Frank Mugogo 9825

UZINDUZI WA MRADI WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU MKOA WA SHINYANGA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Shinyanga. Mgeni rasmi Katika uzinduzi huo uliofanyika tarehe 02/04/2017 katika kijiji cha Negezi Wilaya ya Kishapu alikuwa ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kalemani.

Mradi huu unajumuisha vipengele-mradi vitatu vya Grid Extension, Densification ambayo inalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya vijiji na vitongoji havikuunganishiwa umeme. Kipengele-mradi cha tatu kinahusisha usambazaji wa nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi ambayo ni vigumu kufikiwa na umeme wa gridi.

Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Shinyanga utahusisha vipengele vyote vitatui. Mradi huu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti. Sehemu ya awali itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 149 kwa gharama ya Shilingi Bilioni 35.25. Utekelezaji wa sehemu hii ya kwanza umeanza Mwezi Februari 2017 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 2019.

Aidha, sehemu ya pili ya mradi huu wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu itaanza kutekelezwa baada ya sehemu ya kwanza kukamilika Mwaka 2019 ambapo vijiji 202 vitapatiwa umeme na hivyo kufikisha umeme katika vijiji vyote vya mkoa wa Shinyanga ifikapo Mwaka 2021.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma
S. L. P 7990
Dar es Salaam, Tanzania

Barua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007

Share

Print
«January 2025»
MonTueWedThuFriSatSun
303112345
678
Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Mradi wa Majiko ya Gesi ya Ruzuku Wapokelewa Lindi

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeingia mkataba na mtoa huduma Kampuni ya Taifa Gas Limited kwa ajili ya kutekeleza mradi wa shilingi milioni 317.3 wa kusambaza majiko ya gesi 16,275 (LPG) ya kilo sita kwa bei ya ruzuku ya 50% sawa na shilingi 19,500 kwa jiko katika maeneo ya vijijini Mkoani Lindi.

Read more
9101112
13141516171819
20212223242526
272829303112
3456789

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top