October 28 Announcements Waziri wa Nishati Aweka Ukomo wa Kuagiza Vifaa Vya Ujenzi wa Miradi ya Nishati Announcements, News Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani ameagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme (TANESCO) kuweka mpango ambao utawezesha vifaa vyote vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme vinatengenezwa hapa nchini.
September 28 Announcements Waziri wa Nishati Akutana na Bodi na Wafanyakazi wa Wakala wa Nishati Vijijini Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Merdad Kalemani (Mb) ameagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuwahamasisha wananchi wa vijijini ambako miradi ya kusambaza umeme inatekelezwa kutumia umeme kwa ajili ya kujenga viwanda vya kusindika mali ghafi ambazo zinazalishwa vijijini.
September 20 Announcements Serikali Imetoa Shilingi Billioni 50 kwa Waendelezaji Wadogo Wadogo wa Miradi ya Nishati Jadidifu Serikali imetoa takribani Shilingi Bilioni 50 kwa ajili ya kuwawezesha waendelezaji wadodo wadogo kwenye miradi ya nishati jadidifu, ambazo ni umeme unaozalishwa kutokana na vyanzo vya jua, upepo, maporomoko ya maji pamoja na tungamo taka katika maeneo yaliyopo vijijini Tanzania Bara.
August 10 Announcements Mradi Mpya wa Kusambaza Umeme Pembezoni mwa Miji na Majiji Wazinduliwa Serikali imezindua mradi mpya wa kusambaza umeme kwenye vijiji na mitaa viliyopo pembezoni mwa miji na majiji.Uzinduzi huo umefanyika na Waziri wa Nishati Mh. Dk Medard Kalemani pamoja na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu katika maeneo ya Kigamboni, Kisarawe, Mkuranga, Kibaha, Mlandizi, Bagamoyo na Chalinze.
July 30 Announcements Bodi ya Nishati Vijijini Yapongeza Uzalishaji wa Vifaa vya Miradi ya Umeme Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo amevipongeza viwanda vinavyotengeneza vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kwa uzalishaji wa vifaa kwa kiwango kikubwa unaochochea ukuaji wa sekta ya nishati nchini.
July 20 Announcements Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini Kufanikisha Azma ya Serikali Kujenga Uchumi wa Viwanda Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo amesema miradi ya kusambaza umeme vijijini inayotekelezwa katika wilaya na mikoa yote Tanzania Bara itafanikisha azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo Mwaka 2025.
July 17 Announcements Waziri wa Nishati, Mh. Dk. Merdard Kalemani Aagiza Kuharakisha Utekelezaji wa Miradi ya Kusambaza Umeme Vijijini Waziri wa Nishati Mh. Dk. Merdad Kalemani amewataka wadau wote wanaoshiriki katika utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza kushiriki kikamilifu na kuharakisha utekelezaji wake.
June 21 Tenders REPDF Lot 1 Consultant Database Announcements, Business, News Uploaded is the REPDF Lot 1 Consultant Database.