Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kaskazini Mhe. Francis Kumba Ndulane amewasha umeme katika kijiji cha Nziga Kibaoni Tarafa ya Njinjo katika Jimbo la Kilwa Kaskazini na amepongeza Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa namna ambavyo imeendelea kubadili vijiji kufanana na miji na pia kuweza kuibua fursa mbalimbali za kiuchumi zinazoweza kuwepo kwa kupitia nishati safi na salama.