Social Links Search User Login Menu
Tools
Close
Close
UZINDUZI WA UZINDUZI WA MRADI KABAMBE WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU KIGOMA
Aodax K. Nshala 18464

UZINDUZI WA UZINDUZI WA MRADI KABAMBE WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU KIGOMA

UZINDUZI WA MRADI KABAMBE WA UMEME VIJIJINI AWAMU YA TATU KATIKA MKOA WA KIGOMA NA UKAGUZI WA MIRADI YA UMEME VIJIJINI KATIKA MIKOA YA KATAVI NA RUKWA

Waziri wa Nishati, Mh. Dk, Medard M. Kalemani (Mb) amezindua utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Kigoma na kukag2ua utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini katika Mikoa ya Katavi na Rukwa. Mh. Waziri alifanya uzinduzi huo tarehe 29 Januari, 2018 katika kijiji cha Mabamba, Kata ya Mabamba, Wilaya ya Kibondo.

Mradi huu unajumuisha vipengele-mradi vitatu vya Grid Extension, Densification ambayo inalenga kuongeza wigo wa usambazaji umeme kwenye vijiji ambavyo vimefikiwa na miundombinu ya umeme lakini baadhi ya vijiji na vitongoji havikuunganishiwa umeme. Kipengele-mradi cha tatu kinahusisha usambazaji wa nishati jadidifu kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi.

Utekelezaji wa Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu katika Mkoa wa Kigoma utahusisha vipengele vyote vitatu vya mradi. Mradi huu utatekelezwa kwa vipindi viwili tofauti. Sehemu ya awali itahusisha upelekaji umeme katika vijiji 149 vya Mkoa wa Kigoma kwa gharama ya Shilingi Bilioni 60.5. Utekelezaji wa sehemu hii ya kwanza umeanza Mwezi Februari, 2018 na unatarajiwa kukamilika ifikapo Machi 2019. Katika Mkoa wa Kigoma, utekelezaji wa miradi umegawanywa katika Loti mbili. Loti Na. 1 inahusu Wilaya za Kibondo na Kakonko. Loti Na.2 inahusu Wilaya za Kasulu, Buhigwe, Kigoma Vijijini na Uvinza. Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa Loti Na. 1 ni M/s Urban & Rural Engineering Services Ltd. Wizara ipo katika hatua za mwisho za kumpata Mkandarasi wa Loti Na.2. Mchakato wa manunuzi utakapokamilika, Mkandarasi huyo ataanza kazi mara moja.

Aidha, sehemu ya pili ya mradi huu wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu itaanza kutekelezwa baada ya sehemu ya kwanza kukamilika ifikapo Mwezi Machi 2019 ambapo vijiji 91 vya Mkoa wa Kigoma vitapatiwa umeme na hivyo kufikisha umeme katika vijiji vyote ifikapo Mwaka 2021.

Tahere 30 Januari, 2018, Mh. Waziri wa Nishati alikagua miradi ya umeme vijijini katika Mkoa wa Katavi. Alianza kwa kukagua mradi wa ujenzi wa kituo cha kufua umeme kilichopo Mjini Mpanda . Akiwa Mjini Inyonga, katika Wilaya ya Mlele, Mh. Waziri alikagua ujenzi wa kituo cha kufua umeme kwa ajili ya matumizi katika wilaya hiyo. Pia Mh. Waziri aliwahutubia wananchi wa Wilaya ya Mlele na kuwaeleza taratibu za utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Umeme Vijijini ikiwa ni pamoja na taratibu za kuunganisha kwenye nyumba. Pia Mh.Waziri alifafanua gharama na mfumo wa kulipia miradi ya umeme vijijini wakati wa utekelezaji wa mradi na baada ya kukamilika utekelezaji wa miradi hiyo.

Tahere 31 Januari, 2018, Mh. Waziri wa Nishati alikagua miradi ya umeme vijijini katika Mkoa wa Rukwa. Kwa nyakati tofauti, Mh. Waziri aliwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ntendo, Wilaya ya Sumbawanga Mjini na kuwaeleza taratibu za utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Umeme Vijijini ikiwa ni pamoja na taratibu za kuunganisha kwenye nyumba. Pia Mh.Waziri alifafanua gharama na taratibu za kulipia ili kuunganishwa na huduma ya umeme kwenye miradi ya umeme vijijini wakati wa utekelezaji wa mradi na hata baada ya kukamilika utekelezaji wa miradi hiyo.

Mh. Waziri alihitimisha kwa kuwahutubia wananchi wa Kijiji cha Miangalua, Wilaya ya Sumbawanga Vijijini. Kama alivyohutubia sehemu za awali, Mh. Waziri aliwaeleza wananchi taratibu za utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Umeme Vijijini ikiwa ni pamoja na taratibu za kuunganisha kwenye nyumba. Pia Mh.Waziri alifafanua gharama na taratibu za kulipia ili kuunganishwa na huduma ya umeme kwenye miradi ya umeme vijijini wakati wa utekelezaji wa mradi na hata baada ya kukamilika utekelezaji wa miradi hiyo.

Imetolewa na:

Mkurugenzi Mkuu
Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
Mawasiliano Towers, Ghorofa ya 2
Barabara ya Sam Nujoma
S. L. P 7990
Dar es Salaam, Tanzania

Barua Pepe: info@rea.go.tz
Simu: +255 22 2412001, +255 22 2412002, +255 22 2412003
Nukushi: +255 22 2412007

Share

Print
«September 2026»
MonTueWedThuFriSatSun
31123456
789
Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

Rea Yawajengea Uwezo Waendelezaji wa Miradi Midogo ya Umeme Unaozalishwa na Maporomoko ya Maji

IRINGA, Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuchukua hatua madhubuti katika kuimarisha upatikanaji wa nishati nchini kwa kuendesha mafunzo maalum ya wiki moja yaliyolenga kujenga uwezo wa waendelezaji wa miradi midogo ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower).

Mafunzo hayo yaliyoanza tarehe 7 Septemba, 2026 katika Hoteli ya Sunset mkoani Iringa, yamewakutanisha waendelezaji wa miradi (Developers) zaidi ya 15, hususan kutoka maeneo ya Nyanda za Juu Kusini. Lengo kuu ni kuwajengea uwezo wa kiufundi ili kuongeza ubora wa miradi yao ili iweze kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, tarehe 9 Septemba, 2026, Kaimu Meneja wa Usaidizi wa Kiufundi kwa Waendelezaji Miradi kutoka REA, Mhandisi Emmanuel Yesaya, alisema kuwa REA haishii tu kutoa msaada wa upatikanaji wa nishati vijijini, bali inajikita pia katika kuongeza ujuzi wa wataalamu wa ndani.

"Kuongeza ujuzi kwa waendelezaji hawa kutasaidia kuhakikisha miradi inatekelezwa kwa kuzingatia viwango vya kitaalamu na ubora unaohitajika. Hatua hii itaongeza idadi ya miradi inayofikia vigezo vya kuunganishwa kwenye Gridi ya Taifa, kuongeza uzalishaji wa umeme, na kuchochea maendeleo ya kiuchumi na kijamii vijijini," alisema Mhandisi Yesaya.

Mafunzo hayo yameendeshwa kwa ushirikiano kati ya REA na Wataalamu kutoka Ndaki ya Uhandisi na Teknolojia (CoET) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Maeneo yaliyofundishwa ni pamoja na usanifu wa miradi, upembuzi yakinifu, sayansi ya maji (hydrology), uhandisi wa umeme na elektroniki, pamoja na uendeshaji na matengenezo ya mitambo.

Mbali na mafunzo, REA imebainisha kuwa imekuwa ikisaidia waendelezaji hao kupitia ruzuku za ujenzi, maandalizi ya maandiko ya miradi na usanifu.

Aidha, Wakala huo upo katika mchakato wa kuandaa mfumo wa mikataba ya muda mrefu (Framework Contract) na taasisi za elimu ili kutoa mafunzo endelevu kwenye nishati jadidifu ikiwemo nishati ya jua na mifumo ya gesi vunde.

Kwa upande wao, baadhi ya washiriki wamepongeza mafunzo hayo; akizungumza na Wanahabari, Mhandisi Denis Makoyi kutoka kampuni ya Africa Power Investment, alisema mafunzo hayo yameongeza uelewa mkubwa wa kiufundi katika hatua za utekelezaji wa miradi. Naye Lutengano Kigola kutoka mradi wa Nyalawa Hydropower, aliongeza kuwa mafunzo hayo yanathibitisha kuwa Tanzania ina wataalamu wa ndani wenye uwezo mkubwa wa kuendeleza miradi ya umeme wa maji.

  • MWISHO –

 

Read more
10111213
14
REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

REA Yaendelea Kuwezesha Miradi ya Umeme wa Maji Nyanda za Juu Kusini

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeendelea kuwezesha waendelezaji wadogo wa miradi ya uzalishaji wa umeme unaotokana na maporomoko ya maji (Small Hydropower) katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kwa kutoa fedha, msaada wa kitaalamu na mafunzo, hatua inayolenga kuongeza uzalishaji wa nishati nchini.

Read more
151617181920
21222324252627
2829301234
567891011

Archive

Contact Us

E-Mail
General Information:  info@rea.go.tz
Director General:  dg@rea.go.tz
Procurement (PMU):  pmu@rea.go.tz
Webmaster:  webmaster@rea.go.tz

Mailing Address

Director General
Rural Energy Agency - REA
REA Building
28 Medeli Street
P. O. Box 2153
Dodoma, Tanzania

Phone & Fax

Tel: +255 26 2323504, +255 26 2323506
+255 26 2323507
Fax: +255 26 2323507

Time Zone

Please note that we are based in Tanzania, Time zone (GMT+03:00). Although we may not be in office at times convenient for all international enquiries, we do monitor our e-mail outside normal office hours.

Back To Top