Wakala wa Nishati Vijijini (REA) unaendelea na jitihada mbalimbali za uelimishaji, uhamasishaji na usambazaji wa bidhaa za Nishati Safi za Kupikia katika Mikoa yote Tanzania Bara kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha 80% ya Wananchi wanatumia Nishati Safi za Kupikia ifikapo Mwaka 2034.