Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi ya Bodi ya Nishati Vijijini, Mhandisi Styden Rwebangira amewaagiza Wakandarasi wanaotekeleza Mradi wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya III Mzunguko wa I kuwaunganisha wananchi kwa kutumia kifaa cha Umeme Tayari (UMETA) ambacho ni mbadala wa kufanya wiring katika nyumba.
Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Merdad Kalemani ameagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na Shirika la Umeme (TANESCO) kuweka mpango ambao utawezesha vifaa vyote vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme vinatengenezwa hapa nchini.
Waziri wa Nishati Mh. Dkt. Merdad Kalemani (Mb) ameagiza Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuwahamasisha wananchi wa vijijini ambako miradi ya kusambaza umeme inatekelezwa kutumia umeme kwa ajili ya kujenga viwanda vya kusindika mali ghafi ambazo zinazalishwa vijijini.
Serikali imetoa takribani Shilingi Bilioni 50 kwa ajili ya kuwawezesha waendelezaji wadodo wadogo kwenye miradi ya nishati jadidifu, ambazo ni umeme unaozalishwa kutokana na vyanzo vya jua, upepo, maporomoko ya maji pamoja na tungamo taka katika maeneo yaliyopo vijijini Tanzania Bara.
Serikali imezindua mradi mpya wa kusambaza umeme kwenye vijiji na mitaa viliyopo pembezoni mwa miji na majiji.Uzinduzi huo umefanyika na Waziri wa Nishati Mh. Dk Medard Kalemani pamoja na Naibu Waziri wa Nishati Mh. Subira Mgalu katika maeneo ya Kigamboni, Kisarawe, Mkuranga, Kibaha, Mlandizi, Bagamoyo na Chalinze.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini, Wakili Julius Kalolo amevipongeza viwanda vinavyotengeneza vifaa vinavyotumika katika ujenzi wa miundombinu ya miradi ya usambazaji wa umeme vijijini kwa uzalishaji wa vifaa kwa kiwango kikubwa unaochochea ukuaji wa sekta ya nishati nchini.
Mwenyekiti wa Bodi ya Nishati Vijijini (REB), Wakili Julius Kalolo amesema miradi ya kusambaza umeme vijijini inayotekelezwa katika wilaya na mikoa yote Tanzania Bara itafanikisha azma ya Serikali ya kufikia uchumi wa kati kupitia sekta ya viwanda ifikapo Mwaka 2025.
Waziri wa Nishati Mh. Dk. Merdad Kalemani amewataka wadau wote wanaoshiriki katika utekelezaji wa Mradi Kabambe wa Kusambaza Umeme Vijijini Awamu ya Tatu Mzunguko wa Kwanza kushiriki kikamilifu na kuharakisha utekelezaji wake.