July 16 Announcements KONGAMANO LA “BIG RESULTS NOW” MIRADI MIKUBWA YA NISHATI YATAJWA Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Prof. Sospeter Muhongo, ametaja miradi ya kipaumbele itakayotoa matokeo ya haraka ifikapo 2015/2016, na kunufaisha wananchi katika mikoa mbalimbali nchini. Prof. Muhongo aliitaja miradi hiyo mikubwa jijini Dar es Salaam mbele ya wadau waliokusanyika katika kongamano la wazi la siku moja kwa lengo la kukusanya maoni kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo.
June 28 Announcements SMART PARTNERSHIP INTERNATIONAL DIALOGUE Announcements Watanzania tujitokeze kumuunga mkono Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika Mkutano utakaofanyika Dar es Salaam kuanzia tarehe 28 Juni, 2013 hadi 01 Julai, 2013 maarufu kama SMART PARTNERSHIP INTERNATIONAL DIALOGUE.
June 28 Announcements MPANGO WA KULETA MATOKEO MAKUBWA SASA KWA WIZARA YA NISHATI NA MADINI Announcements Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter Muhongo (Mbunge), anawaalika wadau wote wa Sekta ya Nishati na Madini kote nchini kwenye kongamano la wazi litakalofanyika siku ya Jumatano Julai 3, 2013 kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Mwenge Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3.00 asubuhi hadi saa 11.00 jioni.
May 25 Speeches HOTUBA YA BAJETI YA WIZARA YA NISHATI NA MADINI: MAPATO NA MATUMIZI KWA MWAKA 2013-14 Announcements, Reports, Speeches Hotuba ya Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Sospeter M. Muhongo (Mb.), akiwasilisha Bungeni makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka 2013/14.
May 25 Reports Orodha ya Miradi ya Umeme Vijijini kwa Mwaka wa Fedha 2013-14 Announcements, Reports Orodha miradi ya awamu ya pili ya mradi kabambe wa kusambaza umeme vijijini ambayo inategemewa kupata ufadhili wa mfuko wa nishati vijijini kwa mwaka wa fedha 2013/14.
May 22 Tenders TOR: CONSULTING SERVICES FOR RESTRUCTURING OF INPUT TO RESULT BASED MANAGEMENT SYSTEMS Business Following the formulation of the National Energy Policy in 2003, and the enactment of the Rural Energy Act in 2005, the Rural Energy Board (REB), Rural Energy Agency (REA) and Rural Energy Fund (REF) were established in 2007. REA is the executive body and Secretariat to the REB. The Fund is the mechanism by which the Board shall fulfill its mandate to provide grants and technical support to projects that are developed by private and public entities, co-operatives, and local community organisations.
May 16 Press Releases FAIDA YA GESI ASILIA MIKOA YA LINDI NA MTWARA Gesi asilia iligunduliwa kwa mara ya kwanza hapa nchini Mwaka 1974 kwenye Kisiwa cha Songo Songo, Mkoani Lindi. Ugunduzi mwingine umefanyiaka katika maeneo ya Mtwara Vijijini (Mnazi Bay, 1982 na Ntorya, 2012), Mkuranga (Pwani, 2007) na Kiliwani (Lindi, 2008). Kiasi cha gesi asilia iliyogunduliwa katika maeneo haya inakadiriwa kuwa futi za ujazo trilioni 8. Katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, kumekuwa na kasi kubwa ya utafutaji mafuta na gesi asilia uliojikita zaidi kwenye maji ya kina kirefu cha bahari. Kiasi cha gesi asilia iliyogunduliwa katika kina kirefu cha maji ni takribani futi za ujazo trilioni 33.7. Jumla ya gesi asilia iliyogunduliwa nchi kavu na baharini inafikia takribani futi za ujazo trilioni 41.7.
May 15 News UJERUMANI KUSHIRIKIANA NA SERIKALI YA TANZANIA KATIKA UZALISHAJI WA UMEME VIJIJINI Serikali imesema ipo tayari kushirikiana na Ujerumani katika kuzalisha umeme vijijini kwa kutumia nishati mbadala hususan upepo na jua. Hayo yalisemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Mhe.Profesa Sospeter Muhongo alipokutana na Ujumbe wa Wabunge kutoka Ujerumani.